" Rostam Azizi: Tuimarishe Majukwaa Yetu ya Habari Kabla Taifa Halijasimuliwa na Wengine

Rostam Azizi: Tuimarishe Majukwaa Yetu ya Habari Kabla Taifa Halijasimuliwa na Wengine


Na Zulfa Fadhili, Misalaba Media, Arusha.Mwakilishi wa vyombo vya habari binafsi nchini Rostam Azizi ameonya mijadala mingi kuhusu Tanzania kuendeshwa na watu walioko nje ya nchi ambao hawawajibiki kwa athari za maudhui yao.Akizungumza Katika kongamano la pili la Mabaraza Huru ya Habari Afrika leo Jijini Arusha amesema Tanzania inapaswa kumiliki majukwaa ya kidijitali yenye uwezo wa kushindana kimataifa huku akitoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika miundombinu ya habari kama njia ya kulinda uhuru wa kifikra na kuimarisha maudhui ya kitaifa.Rostam pia amehimiza uwekezaji katika rasilimali watu hasa vijana wanaohitaji mafunzo ya habari za kidijitali na teknolojia ya AI ili waweze kueleza historia ya Tanzania kwa usahihi, uadilifu na muktadha wa ndani kwa kuwa teknolojia mpya ikiwemo mitandao ya kijamii na akili bandia (AI) imeathiri usambazaji wa habari."Tasnia ya habari si ya wachache bali ni sehemu ya uhai wa taifa, hivyo nitoe rai kwa serikali, sekta binafsi na asasi za kiraia kushirikiana kuijenga upya sekta hii kwa kuzingatia hali halisi ya dunia ya leo, tuwe na akili ya kuibadilisha ili ikabiliane na zama za sasa."Akizungumzia historia ya vyombo binafsi nchini amesema ni sehemu ya mabadiliko ya kisiasa na kijamii yaliyoanza miaka ya 1990.Amesema katika miaka ya mwanzo ya mabadiliko ya kisiasa nchini pamoja na kurejea kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kulikwenda sambamba na kuibuka kwa vyombo vya habari binafsi.Mkutano huo wa siku nne umefunguliwa leo na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango ambao unalenga kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuboresha sheria za habari na mawasiliano barani Afrika, kukuza umahiri wa uandishi wa habari kupitia viwango thabiti pamoja na kuonyesha athari za kazi za habari katika jamii.

Post a Comment

Previous Post Next Post