" Simba Yapigwa Faini na Bodi ya Ligi Kisa Dabi na Yanga...

Simba Yapigwa Faini na Bodi ya Ligi Kisa Dabi na Yanga...

 

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Julai 15, 2025 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kuiadhibu klabu ya Simba kwa kuitozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kushindwa kuhudhuria mkutano wa wanahabari kwenye ukumbi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dar es Salaam Juni 24, 2025 kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:58 ya
Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Aidha Simba imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kushindwa kuhudhuria kikao cha kitaalam cha maandalizi ya mchezo (MCM) Juni 24, 2025 kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:2(2.2) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Vilevile Klabu ya Simba imeadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kupitia mlango usio rasmi kuelekea mchezo tajwa hapo juu Juni 25, 2025, kinyume na matakwa ya kanuni ya 17:21 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Post a Comment

Previous Post Next Post