" CCM YAPITISHA MEYA NA NAIBU MEYA JIJI LA MWANZA

CCM YAPITISHA MEYA NA NAIBU MEYA JIJI LA MWANZA

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
MCHAKATO wa kumpata Meya wa Jiji la Mwanza na naibu wake umekamilika baada ya aliyekuwa meya kwa mwaka 2020 hadi 2025 Constantine Sima kuibuka kidedea kwa kupata kura 15 na Anita Rwezaura aliyepata kura 14 akichomoza kama Naibu.Katika kinyang'anyiro cha nafasi umeya iliyofanyika Leo katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Nyamagana Sima diwani wa Kata ya Mhandu, meya wa Jiji hilo kwa awamu iliyopita alimbwaga Happiness Ibasa diwani wa Kata ya Nyegezi alipata kura 11.Awali jumla ya madiwani 10 waliomba ridhaa ya kuchaguliwa kwenye chama chao kwenye nafasi ya meya, hata hivyo yalirudishwa majina ya madiwani wawili kuchuana kwenye kiti hicho kikuu kwenye Baraza la Madiwani.Katika upande wa Naibu Meya Anita Rwezaura diwani viti Maalumu kutoka Nyamagana aliibuka kidedea baada ya kupata kura 14 huku wapinzani wake mmoja alipata kura 3, mwingine 6 na wa tatu 6.Akizungumza baada ya kupata ushindi huo Meya wa Jiji aliwashukuru madiwani wenzake pamoja na mbunge kwa kumuamini kwa awamu ya pili kuhudumia kwenye nafasi hiyo ya juu katika halmashauri ya Jiji la Mwanza."Nina ahidi kuwatumikia wananchi kwa juhudi kubwa ili kutatua  changamoto ya miundombinu, huduma za afya na shule" alisema Sima.Meya huyo mteule aliahidi kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni kuhakikisha suala la miundombinu analipa kipaumbele ili kuhakikisha kuwa changamoto inayotokana na ubovu wa mabarabara inaisha katika kipindi hiki. Zoezi hilo kwa upande wa chama limehitimishwa ambapo kesho watakutana ili waweze kuidhinishwa na Baraza la Madiwani kabla ya kuanza kazi rasmi huku vilevile uapisho kwa madiwani nao utafanyika ukumbi wa mikutano kwenye halmashauri ya Jiji la Mwanza.

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post