Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mh: Mabala Mlolwa leo Desemba 16, 2022
ameongoza shughuli za kufunga kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani
kata ya Mwamalili Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Chama hicho kilizindua
kampenzi za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Mwamalili Desemba 10, 2022 ambapo
leo shughuli ya kufunga kampeni hizo zimehughuriwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga pamoja na Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri
Mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu,Paschal
Patrobas katambi.
Akizungumza mgeni rasmi
kwenye shughuli za kufunga kampeni, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mh:
Mabala Mlolwa ameendelea kuwaomba wakazi wa kata ya Mwamalili kumchagua mgombea
wa CCM Bwana James Mdimi ili aweze kuwasaidia
kutatua changamoto zilizopo kwenye kata hiyo.
Mwenyekiti Mabala amewasisitiza
wakazi wa kata hiyo siku ya kesho kwenda kumpigia kura mgombea wa CCM James
Matinde Mdimi ili aweze kushirikiana na viongozi wengine wa chama na serikali
kwa kuhakikisha ilani ya uchaguzi inatekelezwa kikamilifu.
“Mimi
niwaombe sana wananchi wa Mwamalili siku ya kesho Jumamosi kachagueni ndugu
yetu James Mdimi kampigieni kura za kutosha asubuhi halafu unasubiria matokeo
jioni saa kumi na moja”.amesema Mwenyekiti Mabala
Kwa upande wake mgombea
wa nafasi ya udiwani kata ya mwamalili
Bwana James Matinde Mdimi naye
ameendelea kuwaomba wananchi kumchagua ili aweze kutatua changamoto zilizopo
kupitia sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji na miundombinu ya Barabara.
“Wananchi
wa Mwamalili mimi ni motto wenu nagombea nafasi ya udiwani kata hii nawaomba
kura zenu mama zangu, baba zangu na watu wote ili mnitumie niweze kusimamia
maendeleo ya kata hii hasa vipaumbele vyangu ni kushughulikia changamoto ya
umeme, maji, afya na barabara ambavyo ni kero katika kata ya Mwamalili”.amesema
James Mdimi
Viongozi mbalimbali wa
CCM ngazi ya Mkoa na wilaya nao wamewaomba wananchi wa kata ya Mwamalili
kumchagua James Mdimi katika nafasi ya
udiwani ili ashughulikia kero zao.
Wakizungumza pia Baadhi
ya madiwa kutoka kata mbalimbali za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamewaomba
wakazi wa kata ya mwamalili kuungana na
mgombe wa CCM huku Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mh; Elias Ramadhan
Masumbuko akiwaomba wakazi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi ili kumpigia kura
James Mdimi aweze kushirikiana na madiwani wengine wa Halmashauri ya Manispaa
ya Shinyanga.
Aidha Mbunge wa jimbo la
Shinyanga Mjini Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu,Paschal Patrobas katambi
pamoja na Mbunge viti maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava nao
wametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wakazi wa kata ya Mwamalili kumchagua
Mgombea wa CCM Bwana James Mdimi ili aweze kuleta mabadiliko chanya ya
kimaendeleo.
Chama cha Mapinduzi CCM
Wilaya ya Shinyanga Mjini leo kimefunga kampeini
za uchaguzi mdogo wa nafasi ya udiwani katika kata ya Mwamalili,Jimbo la
Uchaguzi la Shinyanga Mjini ambapo siku ya kesho Jumamosi wakazi wa kata hiyo
watapiga kura kumchangua diwani wao.
Uchaguzi huo mdogo wa nafasi ya udiwani katika kata ya Mwamalili unafanyika kuziba pengo la aliyekuwa diwani wa kata hiyo Paulo Machela ambaye alifariki Dunia Mwanzoni mwa Mwaka huu 2022.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mh: Mabala Mlolwa akizungumza katika shughuli ya kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa diwani kata ya Mwamalili.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana, ajira na wenye ulemavu,Paschal Patrobas katambi akizungumza kwenye shughuli hiyo.
Mbunge viti maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava akiwaomba wakazi wa kata ya Mwamalili kumchagua Bwana James Mdimi katika nafasi ya udiwani kata hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donard Magesa akizungumza kwenye kampeni hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mh; Elias Ramadhan Masumbuko akiwaomba wakazi wa kata ya Mwamalili kujitokeza kwa wingi kwenda kumpigia kura za ndiyo Bwana James Mdimi.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Esther Makune akiwaomba wananchi kumpigia kura za ndiyo mgombea wa CCM Bwana James mdimi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Magile Anold Makombe akizungumza kwenye kampeni hizo.
Diwani wa kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Mh: Hassan Mwendapole akiwaomba wakazi wa kata ya Mwamalili kumchagua mgombea wa CCM James Mdimi.
Diwani wa kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mh: Mussa Elias akiwaomba wakazi wa kata ya Mwamalili kumpigia kura za ndiyo mgombea wa CCM James Mdimi.
Diwani wa kata ya Ngokolo Mh: Victor Mkwizu akimuombea kura mgombea wa CCM Bwana James mdimi.
Diwani wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Zamda Shaban akiwaomba wananchi wa kata ya Mwamalili kumchagua mgombea wa CCM Bwana james Mdimi.
Diwani viti maalum kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga akiwaomba wakazi wa kata ya Mwamalili kumchagua mgombea wa CCM James Mdimi.
Mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya Mwamalili kupitia chama cha mapinduzi CCM Bwana James Mdimi akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo.
Post a Comment