Mkazi wa Nyankumbu mjini Geita, Abdiel Rafael (42) ambaye anadaiwa kuwa ni mchungaji amefariki dunia baada ya kuingia kwenye maombi ya kufunga huku akiitaka familia yake kutokuwa na wasiwasi hata wasipomsikia kwa kuwa hata akifa atafufuka.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha Rafael anayedaiwa kufariki Desemba 3, 2022 akiwa chumbani kwake na taarifa za kifo hicho zilitolewa Desemba 9 baada ya kutofufuka Desemba 8 kama alivyosema.
“Alifariki Desemba 3, alimuaga mke wake na waumini kuwa atakuwa kwenye maombi maalumu ya kufunga na yataisha Desemba 8 na alidai hata akiitwa asipoitika wasiwe na wasiwasi atafufuka na familia iliendelea na maombi hadi Desemba 8 hafufuki”
“Desemba 9 familia ilitoa taarifa kwenye uongozi wa mtaa maana mwili uliendelea kuharibika, polisi walifika na kuchukua mwili uchunguzi wa madaktari walibaini amekufa siku nyingi na chanjo cha kifo ni kutokula muda mrefu” amesema Kamanda Jongo
Kamanda Jongo amesema Rafael alikuwa akifanyia uchungaji kama mchungaji binafsi na kwamba aliaminisha waumini wake kuwa anauwezo wa kufa na kufufuka kama Yesu na anauwezo wa kuishi bila kula kama Yesu.
“Hii ni imani potofu kama imani nyingine, Yesu ni mmoja tuu ambaye alipewa hiyo hali na Mwenyezi Mungu na atabaki kuwa huyohuyo mmoja tuache kuamini hizo imani ukioteshwa ni mizimu na sio Mungu na mwisho wa siku unapoteza maisha “amesema Kamanda huyo.
Kamanda amesema waumini wa mchungaji huyo wanaendela kuelimishwa kuepuka imani hizo kwani hadi sasa wakihojiwa wanaamini ipo siku atafufuka.
Muumini wa mchungaji huyo Kanyasu John amedai mchungaji huyo aliwaeleza kuwa Mungu alimwambia wakati wa kutangaza neno umefika hivyo awaweke waumini wake kwenye maombi ya muda mrefu na aliwaeleza kuwa anaenda kwenye wakati wa kubadilishiwa mwili ili akafanye kazi ya Mungu.
“Alisema Mungu amemwambia tusiogope tulipoenda kumwangalia tukakuta amebadilika tukaanza kuwaza haya ndio ameambiwa anabadilishiwa mwili? maana eneo la huduma tumeandaa na alisema ana vita vikubwa vya kiroho akawa anakunywa maji mengi”alisema
Mwenyekiti wa mtaa wa Uwanja, Nasoro Cherehani amesema mwili wa mchungaji huyo ulikutwa umeharibika na kuwa mkewe alibaini mumewe amekufa tangu Desemba 3 mwaka huu na walikuwa wanasubiri afufuke.
Mchungaji afariki akiwa kwenye maombi ya kufunga
Rehema Matowo, Mwananchi
Geita. Mkazi wa Nyankumbu mjini Geita, Abdiel Rafael (42) ambaye anadaiwa kuwa ni mchungaji amefariki dunia baada ya kuingia kwenye maombi ya kufunga huku akiitaka familia yake kutokuwa na wasiwasi hata wasipomsikia kwa kuwa hata akifa atafufuka.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha Rafael anayedaiwa kufariki Desemba 3, 2022 akiwa chumbani kwake na taarifa za kifo hicho zilitolewa Desemba 9 baada ya kutofufuka Desemba 8 kama alivyosema.
“Alifariki Desemba 3, alimuaga mke wake na waumini kuwa atakuwa kwenye maombi maalumu ya kufunga na yataisha Desemba 8 na alidai hata akiitwa asipoitika wasiwe na wasiwasi atafufuka na familia iliendelea na maombi hadi Desemba 8 hafufuki”
“Desemba 9 familia ilitoa taarifa kwenye uongozi wa mtaa maana mwili uliendelea kuharibika, polisi walifika na kuchukua mwili uchunguzi wa madaktari walibaini amekufa siku nyingi na chanjo cha kifo ni kutokula muda mrefu” amesema Kamanda Jongo
Kamanda Jongo amesema Rafael alikuwa akifanyia uchungaji kama mchungaji binafsi na kwamba aliaminisha waumini wake kuwa anauwezo wa kufa na kufufuka kama Yesu na anauwezo wa kuishi bila kula kama Yesu.
“Hii ni imani potofu kama imani nyingine, Yesu ni mmoja tuu ambaye alipewa hiyo hali na Mwenyezi Mungu na atabaki kuwa huyohuyo mmoja tuache kuamini hizo imani ukioteshwa ni mizimu na sio Mungu na mwisho wa siku unapoteza maisha “amesema Kamanda huyo.
Kamanda amesema waumini wa mchungaji huyo wanaendela kuelimishwa kuepuka imani hizo kwani hadi sasa wakihojiwa wanaamini ipo siku atafufuka.
Muumini wa mchungaji huyo Kanyasu John amedai mchungaji huyo aliwaeleza kuwa Mungu alimwambia wakati wa kutangaza neno umefika hivyo awaweke waumini wake kwenye maombi ya muda mrefu na aliwaeleza kuwa anaenda kwenye wakati wa kubadilishiwa mwili ili akafanye kazi ya Mungu.
“Alisema Mungu amemwambia tusiogope tulipoenda kumwangalia tukakuta amebadilika tukaanza kuwaza haya ndio ameambiwa anabadilishiwa mwili? maana eneo la huduma tumeandaa na alisema ana vita vikubwa vya kiroho akawa anakunywa maji mengi”alisema
Mwenyekiti wa mtaa wa Uwanja, Nasoro Cherehani amesema mwili wa mchungaji huyo ulikutwa umeharibika na kuwa mkewe alibaini mumewe amekufa tangu Desemba 3 mwaka huu na walikuwa wanasubiri afufuke.
Chanzo - Mwananchi
Post a Comment