Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Chama cha ACT Wazalendo kimezindua kampeni za uchaguzi
mdogo wa nafasi ya udiwani kata ya Mwamalili ambapo kimewaomba wananchi wa eneo hilo kukichagua chama hicho
ili kiweze kuleta mzukumo wa maendeleo katika kata hiyo.
Akizindua kampeni hizo
kupitia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Seseko kata ya Mwamalili mjumbe wa
Halmashauri kuu ya ACT Wazalendo Taifa Bwana Shilungushela Nyangaki amewaomba
wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea wa ACT Wazalendo ili kumpa nafasi ya kuwa
muwakilishi wao kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga.
Bwana Shilungushela
amemuombea kura mgombea wa chama hicho akisema iwapo atachaguliwa ataweka
msukumo wa kuleta maendeleo.
“Ukiwa
hapa Seseko utafikiri siyo Manispaa ni kwa sababu ya kukosa mtetezi makini kwa
sababu mapato ya mjini yanatakiwa yaje huku mboreshewe miundombinu maisha
yatengamae unatakiwa ufikie umeme hapa kuweni waelewa changamkieni fursa hii
iliyojitokeza mjaribu kubadilisha uongozi huyu Joseph Machiya anatosha”.amesema
Shilungushela
Akizungumza katika kampeni hiyo mgombea wa
nafasi ya udiwani kata ya mwamalili
kupitia chama cha ACT Wazalendo Bwana Joseph Yunja Machiya amewaomba
kura wananchi wa kata hiyo ili aweze kushughulikia changamoto zinazowakabili.
“Nawaomba
sana vijana, akina Baba, akiwa Maba na wazee mnipe kura tarehe 17 na jira langu
nila kwaza tu kwenye karatasi ukiona tu picha yangu weka vema kuna kero nyingi
sana za hapa kata ya Mwamalili endapo mkinipa kura nitahakikisha mnapata umeme
na maji yanakuja lakini pia changamoto zote mtanituma na nitazifikisha kingine
nitahakikisha kila baada ya miezi mitatu nafanya mkutano wa hadhara”.amesema
Joseph Machiya
Aidha viongozi
mbalimbali wa chama cha ACT Wazalendo
ngazi ya Mkoa na wilaya wametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa kata
ya Mwamalili kumchagua mgombea wao Joseph Machiya katika nafasi ya udiwani.
Wakati huo huo baadhi
ya wananchi wa kata ya Mwamalili wamesema wanahitaji kupata mwakilishi mwenye
sifa za kiongozi bora katika nafasi hiyo ya udiwani.
Post a Comment