" MIAKA 61 YA UHURU WANANCHI SHINYANGA WAPATWA NA WASI WASI KWENYE MAENDELEO YA MKOA

MIAKA 61 YA UHURU WANANCHI SHINYANGA WAPATWA NA WASI WASI KWENYE MAENDELEO YA MKOA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wakazi wa mkoa wa Shinyanga  wamesema Miaka 61 ya uhuru serikali inapaswa kuongeza kasi ya kuleta maendeleo ili Mkoa uweze kufanana na rasilimali zilizopo.

Wamesema licha ya kufikiwa kwa mafanikio mbalimbali lakini Mkoa wa Shinyanga umedumaa kimaendeleo ikilinganishwa na rasilimali zilizopo ikiwemo Mifugo, kilimo cha mazao ya biashara pamoja na madini ya almas

Wameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na Misalaba Blog  kama sehemu ya maadhimisho ya Miaka 61 ya uhuru ambapo wameomba serikali iongeze kasi ya uboreshaji wa huduma za kijamii kwenye eneo la miundombinu.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga (RSA) Seif Nasolo amewapongeza viongozi viongozi wa Mkoa na Wilaya kwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi hali ambayo imesaidia au kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wameahidi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura katika uboreshaji wa miundombinu mbalimbali hali ambayo inaleta madhari nzuri ya Mji wa Shinyanga. 

 

Mwenyekiti wa usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga (RSA) Seif Nasolo wakati akipongeza juhudi za serikali kupitia viongozi mbalimbali.


Post a Comment

Previous Post Next Post