" MKUU WA MAGEREZA MKOA WA SHINYANGA SEMWENDA AKUMBUSHA KUFANYA KAZI KWA BIDII, NI MIAKA 61 YA UHURU

MKUU WA MAGEREZA MKOA WA SHINYANGA SEMWENDA AKUMBUSHA KUFANYA KAZI KWA BIDII, NI MIAKA 61 YA UHURU

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Magereza Josephine Semwenda amesema Miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika, watanzania waongeze juhudi katika kazi kama kielelezo cha kuunga mkono  dhamira ya serikali inayolenga kuwa na Taifa lenye uchumi imara.

Amesema mafanikio mbalimbali yaliyopo yametokana na mifumo thabiti iliyowekezwa,  ikiwemo kufanya kazi halali kwa juhudi na maarifa ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Misalaba Blog ofisini kwake kuelekea siku ya Uhuru wa Tanganyika kesho Disemba 09, ambapo amesema mafanikio yanayoonekana hivi sasa iwe ni kichocheo cha watanzania wote, kuongeza juhudi na maarifa katika kazi na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo Biashara, Kilimo na ujasiliamali.

“Tunafanya jambo jema sana tunapokumbuka siku yetu ya uhuru na tunafanya kila Mwaka ili kuenzi siku yetu ya uhuru kwanza tunafura lakini pili tunarithisha kizazi chetu watoto wetu, wajukuu wetu wajue kwamba kumbe Nchi yetu  tulipataga uhuru siku furani”.amesema RPO Semwenda

“Nawashauri watanzania wenzangu tufanye kazi kwa bidii tumuunge mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan maana anafanya kazi sana, anahangaika sana kutuletea pesa ametuletea ajira basi mtu unapopata ajira fanya kazi kwa tija na ufanisi lakini pia tufanye kazi kwa kuepuka rushwa tufanye kazi kwa haki tukifanya hivyo tutakuwa tumemuunga mkono Rais  Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.amesema RPO wa Shinyanga Semwenda

RPO Semwenda amesema Miaka 61 ya  uhuru Tanzania licha ya changamoto kadhaa zilizopo lakini kwa kiwango kikubwa, Nchi imepiga hatua  za mafanikio katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya uchukuzi hasa katika eneo la uboreshwaji wa miundombinu.

Mkuu huyo wa Magereza Mkoa wa Shinyanga RPO Semwenda amesema taasisi hiyo itaadhimisha siku ya uhuru wa Tanganyika kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii  ikiwemo usafi wa Mazingira.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post