Mkuu wa Wilaya ya
Shinyanga Jasinta Mboneko amewataka wazazi kuhakikisha Watoto wote wanaotakiwa
kwenda shule kwa Mwaka wa Masomo 2023,wanaripoti shuleni kwa wakati.
Ameyasema hayo leo wakati
akizungumza na Misalaba Blog ofisini kwake ambapo amewaomba wakuu wa shule
pamoja na walimu wengine kutoweka vikwazo vyovyote kwa watoto wanaotakiwa
kwenda shuleni huku akiwasisitiza
wanawapokea bila kujali changamoto zao.
DC Mboneko
amewasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa watoto
ikiwemo kuwanunulia sale za shule, vifaa na mahitaji mengine ili wasome kwa
bidii na kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.
“Nitoe
wito kwa viongozi wote kwenye ngazi zetu za vitongozi, vijiji, mitaa, kata na
Wilaya kwa ujumla kuhakikisha kwamba watoto wote wanaotakiwa kuwa shuleni
wawepo shuleni lakini pia kwa watoto ambao wameandikishwa kuanzia darasa la
awali na darasa la kwanza”.
“
Nitoe wito kwa wakuu wa shule pamoja na walimu wengine kwamba tusiweke urasimu
wowote kwa watoto ambao wanatakiwa wawe shuleni na jambo hili katika baadhi ya
maeneo tayari limeshasikika kuna urasmi ambao unawekwa na walimu kwamba watoto
hawa wasipokelewa kwa sababu hawana sale, hawana viatu, hawana vifaa vya shule
mimi niwahimize wazazi na walezi tujitahidi kuwanunulia mahitaji ya shule
watoto wetu ili waende shuleni lakini pia na wale wa awali na darasa la kwanza
wanaweza kuanza na nguo za nyumbani”.amesema DC Mboneko
Mboneko amesema tangu
shule zifunguliwe hakuna changamoto iliyojitokeza ambapo amempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan huku akieleza kuwa shule
zote za Wilaya ya Shinyanga zinaendelea vizuri na zoezi la kupokea wanafunzi.
Dc Mboneko amekumbusha viongozi kuanzia ngazi ya Mtaa, wanafunzi, wazazi na
walezi pamoja na jamii kwa ujumla kutofumbia macho taarifa za ukatili, na kwamba wanapaswa kutoa
taarifa kwa wakati sehemu husika ili hatua zaidi zichukuliwe.
“Suala
la kumlinda mototo na ukatili nila wote siyo serikali tu jamii pia inapaswa
kushirikiana na serikali lakini niwaombe wazazi wawe na utamaduni wa kukaa na
kuzungumza na watoto wao hii desturi itasaidia wazazi kujua hali ya mototo wake
kila siku”. amesema DC Mboneko
“Watoto,
wazazi na walezi pamoja na jamii linapotokea suala hili la ukatili wa kijinsia
basi litolewe taarifa haraka sana ili hatua za kisheria zichukuliwe, utakuta
mtu amefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ameshaoga ametoa kila kitu na
huwezi tena kupata ushahidi kwahiyo niombe sana linapotokea jambo hili litolewa
taarifa haraka mtu asifiche taarifa hata kama ni kiongozi wa eneo husika
ameshiriki kwa namna moja ama nyingine tutamchukulia hatua”.
“Wazazi
na walezi pia waendelee kufuatilia masuala yote ya elimu kwa watoto wao kwamba
wanakwenda shuleni na wanarudi nyumbani salama lakini pia wazazi waache tabia
ya kuozesha watoto niwatake wasubiri mpaka ufike ule umri wao wa kwenda kuolewa
ndiyo waolewe kwa sababu ukatili mwingine unafanyika ndani ya familia na nje ya
familia lazima tuwajengee watoto uwezo wa kutoa taarifa kwahiyo ni vizuri sana
wazazi wakawa na utamaduni wa kuongea na watoto wao”.
amesema DC Mboneko
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na Misalaba Blog ofisi kwake leo Ijumaa Januari 13,2023.
Post a Comment