
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, limeombwa kufanya uchunguzi wa
kina ili kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu aliyehusika na tukio la mtoto
wa kike anayesadikika kubakwa mwenye umri wa miaka minne ambaye anasoma chekechea katika Manispaa ya Shinyanga.
Ombi
hilo limetolewa na Familia ya Bwana Paschal Nikolaus
mkazi wa kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga ambapo mlezi wa mtoto huyo Bi.
Anna Salehe Mwarabu amesema tukio hilo limetokea Alhamisi Machi 23, Mwaka huu
2023.
Mlezi huyo Bi. Anna Mwarabu ameelezea
namna mtoto huyo alivyopotea maada ya kutoka shuleni jioni.
‘Mtoto
alitoka shule salama lakini jioni muda wa saa kumi na moja watoto walikuwa
wanacheza cheza Mama yao mkubwa aliwaita akakatuma kale kadogo akakaambia hivi
kamwite yule mwenzako mje muoge kabla ya baridi kuanza kakaenda wenzie wakasema
hayupo Mama yake mkubwa akaenda kumtafuta badaye naye akarudi akasema mtoto
nimemkosa akanishikia mtoto na mimi nikaenda kumtafuta nikazunguka sikumuona
nikawa naelekezwa nenda sehemu furani kaangalie labda wanaosoma naye hamna
sikufanikiwa’
‘Ikabidi
nimpigie Baba yao mdogo alikuwa kazini akasema anakuja mi nikaendelea kutafuta
badaye nikawaita wale watoto aliokuwa akicheza nao nikawaulizaje hivi nyie
mlikuwa mnacheza na mwenzenu mbona kila siku mnacheza naye leo imekuaje
haonekani wakati siyo kawaida yake kale kengine kakasemaje yeye si alikubali kwenda
na lile libaba nikawauliza libaba gani wakasema lilikuwa limekaa pale kwenye
tofali anapokaaga Mama wale watoto wakasema hata sisi lile libaba lilikuwa
linatuita yeye akasema haogopi akaenda likaenda kumkubatia mimi sasa
nikachanganyikiwa na watu wakawa wengi wakaanza kunisaidia kumtafuta ikabidi
nienda kutoa taarifa kwenye mwenyekiti wa mtaa’
‘Baba
yake mdogo mara akanipigia simu akaniambia mtoto tumemuona alikuwa nako jamaa
tu anatembea huku amekashikilia mkono nimemuuliza akasema amemuokota Relini
watu wakawawanamshambulia huyo kijana badaye tukaenda kumweleza Mwenyekiti wa
mtaa’
‘Nilipotoka
kwa mwenyekiti nikaenda kituoni nikamkuta mtoto tukawa tunamhoji hapo badaye
wakasema tukamkague kweli tukaenda kumuangalia ikaonekana mtoto hajachanika ili
ameingiliwa kwa sababu tulikuta zile dalili badaye tukapewa PIOF3 baba yake
mdogo ndiyo aliendelea naye kumpeleka Hospitali waliambiwa warudi tena asubuhi
ya leo ndiyo ameenda tena amebimwa mtoto baadhi ya vipimo ameambiwa atapigiwa
simu’
Mama mlezi wa mtoto Bi. Anna Mwarabu pamoja
na Baba mzazi wa mtoto huyo Bwana George Nikolaus wameiomba serikali kupitia
vyombo vyake kuchunguza kwa kina tukio hilo ili hatua kali za kisheria
zichukuliwe kwa mtu aliyehusika.
Mmoja wa majirani katika familia hiyo
ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema matukio mbalimbali ya namna hiyo hutokea
katika mtaa huo ambapo wazazi hushindwa kutoa ushirikiano kwenye mamlaka husika na kwamba kupitia tukio hilo ameiomba
serikali kuchukua hatua kali kwa mtu atakayebainika kufanya kitendo hicho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa
Bondeni kata ya Masekelo Juma Idd Maloda amekili kupokea taarifa za tukio hilo ambapo
ameeleza kuwa baada ya kufuatilia amebaini kuwa mtu anayedaiwa kuhusika na
tukio hilo ni mtu anayeishi mtaa jirani.
“Mtoto
yule kwa umri wake inaonekana kuna zezeta alikuja kumlagai akamtorosha ndiyo
akaenda kupata zuruba hiyo maana hule mtoto kwa umri wake wa Miaka minne si
rahisi kwenda Ibinzamata peke yake inamaana alichukuliwa inamaana alichukuliwa
kwa sababu hapo kuna mto sisi huwa tunavuka mto kwanza na huwa tunachukua
tahadhari kubwa kwa mtoto kuvuka pale”.
“Tulipopata
tukio hilo tuliwasiliana na Polisi kata lakini hata leo mimi nimeenda polisi
kwenda kujiridhisha na kweli nimemkuta huyo Bwana aliyekuwa amemchukua mtoto
nimemuuliza baadhi ya maswali nikamwuliza unanifahama mimi akasema hapana
unaishi mtaa gani akanitajia mtaa jirani basi tunaliomba tu jeshi la Polisi kama
kweli huyo mtu anahusika sheria ichukue mkondo wake”.amesema
Mwenyekiti wa mtaa Bwana Maloda
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa
Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John amekili kumpokea mtoto
huyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa vipimo vya awali.
Zimefanyika jitihada mbalimbali za kumpata kaimu kamanda wa jishi la Polisi Mkoa wa Shinyanga lakini hazikufanikiwa mpaka sasa.
Mtoto wa kike anayesadikika kubakwa mwenye umri wa miaka minne ambaye anasoma chekechea katika Manispaa ya Shinyanga.
Post a Comment