" CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO CHATIKISA MPIRA WA WAVU KWA KUWADUWAZA WENYEJI DON BOSCO DIDIA.

CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO CHATIKISA MPIRA WA WAVU KWA KUWADUWAZA WENYEJI DON BOSCO DIDIA.

Na Elisha Petro, Misalaba Blog

Timu ya mpira wa wavu (Volleyball) kwa upande wa wavulana  katoka  chuo cha sayansi za Afya Kolandoto kilichopo manispaa ya shinyanga imeishangaza shule ya secondary Don Bosco baada ya ushindi wa jumla ya set 3-0 katika mchezo wa kusisimua uliochezwa katika uwanja wa shule ya secondary don bosco Didia iliyopo halmahsuri ya shinyanga.

Mchezo huo ni miongoni mwa michezo iliyochezwa  katika bonanza la kuimarisha afya,kudumisha ushirikiano, kuinua pamoja na  kuendeleza vipaji kwa washiriki wote kwani michezo ni afya na chanzo cha ajira kwa vijana.

Wachezaji wa chuo cha Kolandoto Halimashauri ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na Shule ya sekondari ya Don Bosco Didia wakiwania mpira katika mchezo wa  mpira wa Wavu.Wakati huohuo katika mchezo wa mpira wa miguu kwa wavulana timu ya chuo cha sayansi za Afya Kolandoto imetoshana nguvu ya kufunganga goli 1-1 dhidi ya wenyeji wao kutoka shule ya sekondari Don Bosco kwa magoli yote kufungwa katika kipindi cha pili baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kutamatika kwa sare ya bila kufungana (suluhu).

Kwa upande wa mpira wa pete Netball wenyeji wa bonanza hilo  shule ya sekondari Don Bosco wamekiduwaza chuo cha sayansi za Afya Kolandoto baada ya kuibuka na ushindi  wa jumla ya goli 18 – 6.

Kwingineko katika mpira wa kikapu basketball wenyeji shule ya sekondari Don Bosco wamewakaribisha wageni wao kutoka chuo cha sayansi za Afya nkolandoto kwa kichapo cha jumla ya vikapu 79 -70 kwenye mchezo uliochezwa kwa  kota nne.

 

Timu ya mpira wa kikapu kutoka chuo cha sayansi za Afya Kolandoto wakitafuta nafasi ya                                               kuwapenya vijana wa shule ya sekondary Don Bosco Didia.

Kaimu mkuu wa chuo cha sayansi za Afya Kolandoto  Michael Henerco kushoto akiwa na Makamu mkuu wa chuo taaluma   Ole Saitabau kulia kwake.Picha mbalimbali za matukio ya bonanza la kuimalisha Afya,kudumisha mshikamano,kuendeleza na kuinua vipaji kwa wanafunzi lililofanyika katika shule ya sekondari Don Bosco iliyopo Halimashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

 

 

 
Wanafunzi wa shule ya sekondary Don Bosco na chuo cha sayansi za Afya kolandoto wakifanya mazoezi  kwa pamoja katika ukumbi wa shule ya sekondary Don Bosco Didia kabla ya michezo kuanza.






Post a Comment

Previous Post Next Post