Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mitihani ya kidato cha sita katika shule mbalimbali za
sekondari Mkoani Shinyanga inaendelea huku wanafunzi wakiahidi kupata matokeo
mazuri.
Misalaba Blog imetembelea katika baadhi ya shule
ikiwemo Buluba sekondari iliyopo Manispaa ya Shinyanga na kuzungumza na baadhi
ya watahiniwa ambapo wamesema tangu kuanza kwa mitihani hiyo Mei 02,Mwaka huu
2023 wameendelea kufanya vizuri kwa mafaniko.
Watahiniwa hao wamesema kutokana na maadalizi mazuri yaliyofanyika
kabla ya mitihani hiyo matarajio yao ni kupata ufaulu mzuri.
Akizungumzia mitihani inayoendelea mkuu wa shule ya
sekondari Buluba mwalimu Robert Charles amewaomba kuendelea kuzingatia taratibu
na kanuni za mitihani ili waweze kuhitimisha zoezi hilo kwa usalama zaidi.
“Mitihani
inaendelea vizuri na sisi tuliwaandaa vizuri na wanatarajia kupata matokeo
mazuri tu, tutamaliza tarehe 12 Mei 5 mtihani wa mwisho utakuwa ni Physics niendelee
tu kuwasihi wazingatia taratibu zote zilizopo na wajiandae tu vizuri kwa
mitihani iliyobaki ili wapate matokeo mazuri tayari kwa kujiunga na chuo kikuu”amesema
Mwalimu Charles
Mitihani ya kidato cha sita katika shule mbalimbali za
sekondari Nchini imeanza Mei 2, 2023 na inatarajiwa kumalizika Mei 12, Mwaka
huu 2023.
Post a Comment