" KAIMU MWENYEKITI SMAUJATA IDARA YA MAKUNDI MAALUM TAIFA BI. KANG’OMBE AMWOKOA MTOTO AKICHUNGA NG’OMBE KISHAPU

KAIMU MWENYEKITI SMAUJATA IDARA YA MAKUNDI MAALUM TAIFA BI. KANG’OMBE AMWOKOA MTOTO AKICHUNGA NG’OMBE KISHAPU

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kaimu Mwenyekiti SMAUJATA idara ya makundi maalum Taifa Bi. Sophia Kang’ombe amefanikiwa kumwokoa mtoto anayekadiliwa kuwa na umri wa Miaka 10 aliyekuwa akifanya kazi ya kuchunga Ng’ombe Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Bi. Sophia Kang’ombe  ameeleza namna alivyoongea na mtoto pamoja  na familia hiyo ambapo  mtoto huyo alikuwa akifanya kazi ya kuchunga Ng’ombe zaidi ya Miezi minne.

“Nimeongea na mtoto akasema yeye anatoka Tabora alikuja na kijana mweziye Kahama kutafuta maisha wakawa wanaokota makopo mitaani na kulala popote badaye alitokea mama mmoja akamchukua akamleta huku Shinyanga Ndoleleji kwa ajili ya kufanya kazi za kuchunga Ng’ombe amechunga zaidi ya miezi minne lakini yule baba wa hiyo familia akamkataa na akapiga simu kwa dada yake kwamba arudi tu nyumbani kwako”

‘Niliendelea  kuongea na yule mtoto mwanzoni alikuwa anakataa kurudi nyumbani kwamba amezoea kuchunga nikaongea na hiyo familia badaye mtoto pia nikawa namwambia arudi nyumbani kwao kulingana na umri wake anatakiwa asome  mimi nikawa namwambia  kwamba ukilazimisha kurudi kwa yule mzee aliyemkataa anaweza kumfanyia ukatili wa aina yoyote anaweza kumpiga, kumchoma moto au kumuua kwa sababu ameshamkataa na mbaya zaidi amefanya kazi hajalipwa hela yoyote ile na mpango wao walikuwa wanataka kumtelekeza yule mtoto eneo la WODI ya wazazi Hospitali ya Kolandoto”.Amesema Bi. Kang’ombe

“Nilifanya juhudi za kumpata mtu wa kumpeleka mtoto huyo Kahama badaye nikampata mama mmoja nikaongea  naye kwamba ampeleke mtoto nyumbani kwao au ampeleke kwenye ofisi za maafisa ustawi wa jamii Kahama ili wawasiliana na wazazi wake waje wamchukue mtoto, yule mama akawa amerithia na yule mtoto nikampa namba yangu ya simu nikamwambia ukipata changamoto yoyote au akikutelekeza tafuta mtu yoyote mwenye simu nipigie nashukuru Mungu wamefika salama tayari taratibu zinafanyika kwa sasa mtoto yuko mikononi mwa Sungusungu”.Amesema Bi. Kang’ombeAidha Bi. Sophia Kang'ombe amesema juhudi za kuwatafuta ndugu zake kwa kushirikiana na viongozi wa serikali pamoja na maafisa ustawi wa jamii Mkoani Tabora ili kumfikisha mtoto kwenye familia ama ndugu zake.Kaimu Mwenyekiti SMAUJATA idara ya makundi maalum Taifa Bi. Sophia Kang'ombe akiongea na mtoto huyo mwenye umri wa Miaka 10 juu ya athari zitokanazo na ukosefu wa elimu.

Post a Comment

Previous Post Next Post