Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kaimu Mwenyekiti SMAUJATA idara ya makundi maalum
Taifa Bi. Sophia Kang’ombe amefanikiwa kumwokoa mtoto anayekadiliwa kuwa na
umri wa Miaka 10 aliyekuwa akifanya kazi ya kuchunga Ng’ombe Wilaya ya Kishapu Mkoani
Shinyanga.
Bi. Sophia Kang’ombe ameeleza namna alivyoongea na mtoto pamoja na familia hiyo ambapo mtoto
huyo alikuwa akifanya kazi ya kuchunga Ng’ombe zaidi ya Miezi minne.
“Nimeongea na mtoto akasema yeye anatoka Tabora alikuja na kijana mweziye Kahama kutafuta
maisha wakawa wanaokota makopo mitaani na kulala popote badaye alitokea mama
mmoja akamchukua akamleta huku Shinyanga Ndoleleji kwa ajili ya kufanya kazi za
kuchunga Ng’ombe amechunga zaidi ya miezi minne lakini yule baba wa hiyo
familia akamkataa na akapiga simu kwa dada yake kwamba arudi tu nyumbani kwako”
‘Niliendelea
kuongea na yule mtoto mwanzoni alikuwa
anakataa kurudi nyumbani kwamba amezoea kuchunga nikaongea na hiyo familia badaye
mtoto pia nikawa namwambia arudi nyumbani kwao kulingana na umri wake anatakiwa asome mimi
nikawa namwambia kwamba ukilazimisha kurudi kwa yule mzee aliyemkataa
anaweza kumfanyia ukatili wa aina yoyote anaweza kumpiga, kumchoma moto au kumuua
kwa sababu ameshamkataa na mbaya zaidi amefanya kazi hajalipwa hela yoyote ile
na mpango wao walikuwa wanataka kumtelekeza yule mtoto eneo la WODI ya wazazi Hospitali ya Kolandoto”.Amesema
Bi. Kang’ombe
Kaimu Mwenyekiti SMAUJATA idara ya makundi maalum Taifa Bi. Sophia Kang'ombe akiongea na mtoto huyo mwenye umri wa Miaka 10 juu ya athari zitokanazo na ukosefu wa elimu.
Kaimu Mwenyekiti SMAUJATA idara ya makundi maalum Taifa Bi. Sophia Kang'ombe wa kwanza upande wa kushoto wakizungumza na mtoto huyo.
Kaimu Mwenyekiti SMAUJATA idara ya makundi maalum Taifa Bi. Sophia Kang'ombe wa kwanza upande wa kushoto wakizungumza na mtoto huyo.
Mama aliyempeleka mtoto Wilayani Kahama baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti SMAUJATA idara ya makundi maalum Taifa Bi. Sophia Kang'ombe.
Post a Comment