" KAMATI YA UTEKELEZAJI JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA SHINYANGA MJINI YAZUNGUMZA NA WANACHAMA CHIBE, NDEMBEZI NA OLD SHINYANGA

KAMATI YA UTEKELEZAJI JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA SHINYANGA MJINI YAZUNGUMZA NA WANACHAMA CHIBE, NDEMBEZI NA OLD SHINYANGA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini imeendelea na ziara zake ambapo leo imetembelea na kukagua uhai wa jumuiya katika kata ya Chibe, Ndembezi pamoja na kata ya Old Shinyanga zilizopo Manispaa ya Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine kamati hiyo imetembelea na kukagua hatua zilizofikiwa katika uboreshaji wa Zahanati ya Chibe ambapo viongozi wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini wameshauri namna bora ya kutatua   changamoto mbalimbali zilizopo kwenye Zahanati hiyo.

Viongozi wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini wamezungumza na jumuiya za wazazi kata ya Chibe, kata ya Ndembezi pamoja na kata ya Old Shinyanga ambapo wamepokea changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo huku wakitoa maelekezo na kuahidi baadhi ya changamoto kuzishughulikia ili kuendeleza umoja wa jumuiya hiyo.

Katika ziara  hiyo Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko amezisisitiza jumuiya hizo kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo itakayowanufaisha wao na jumuiya kwa ujumla.

Mwenyekiti huyo Bwana Mrindoko ameziomba jumuiya hizo kuendelea kushirikiana na viongozi mbalimbali wa chama pamoja na serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.

Amewashukuru kwa kumwamini katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini huku akiwahakikishia wanachama na viongozi kwenye matawi yote kuwa ataendelea kushirikiana nao ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko ametumia nafasi hiyo kuwaasa wazazi kulea watoto kwa kuzingatia mila na distiri za Nchi ili kuwaepusha na mmomonyoko wa maadili.

“Wazazi tunawajibu wa kuwapa elimu watoto wetu juu ya mila na desturi za Nchi hii maana siku hizi wapo wasanii wanaonekana kwenye TV mavazi yao niya aibu na ukifuatilia utakuta wametoka kwenye familia ambayo yupo Baba na Mama sisi jumuiya ya wazazi hatukubaliani na tabia hizo niwaombe wazazi tuwape elimu watoto wetu ili waachane na mila za wengine wafuate mila zetu za Tanzania”.amesema Mwenyekiti Mrindoko

Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Doris Kibabi amewataka wazazi kutoshirikiana na watoto wao juu ya mambo mbalimbali yasiyofaa katika jamii ambayo hupelekea vishawishi vibaya hasa kwa watoto wa kike.

 Katibu huyo pia amesisitiza jumuiya kwenye kata kuendelea kuongeza na kusajiri wanachama wapya huku akikemea makundi mabaya kwenye jumuiya za wazazi kata ya Chibe, Ndembezi na jumuiya ya wazazi kata ya Old Shinyanga.

Naye mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe amewakumbusha wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata elimu stahiki ambapo amesema hali hiyo itasaidia kuwaepusha watoto kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa ambayo hukwamisha mafanikio katika maisha yao ya kila siku.

“Elimu ndiyo kila kitu kwenye Dunia hii kwahiyo tunatakiwa tushirikiana na serikali hasa sisi wazazi kwenye malezi tuhakikishe watoto wanasoma Rais mama Samia anajitahidi sana kuboresha miundombinu ya mazingira ya shule ili watoto waweze kusoma, watoto wakisoma watapata maarifa ya kujiajiri au kuajiriwa ili kuja kusaidia familia kwahiyo usikate tamaa kumsomesha mtoto kwa sababu ya changamoto ndogondogo utashindwa kupata msaada zaidi ukija kuzeeka”. Amesema Mhandisi Jumbe

Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi imeambatana na viongozi wengine akiwemo katibu wa mbunge jimbo la Shinyanga Bwana Samwel Jackson ambapo kamati  hiyo leo Jumamosi Mei 13,2023 imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kukagua uhai wa jumuiya katika kata ya Chibe, Ndembezi pamoja na kata ya Old Shinyanga zilizopo Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akizungumza ikiwa ni sehemu ya ziara kutembelea na kukagua uhai wa jumuiya kwenye kata leo Jumamosi Mei 13,2023.

Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Doris Kibabi akizungumza kwenye kikao cha pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa jumuiya ya wazazi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 13,2023.

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe akizungumzia malezi bora kwa watoto wakati wa ziara hiyo leo Jumamosi Mei 13,2023.

 

Viongozi na wanachama mbalimbali wakiwemo wa jumuiya ya wazazi kata ya Ndembezi wakiwa kwenye kikao cha pamoja na kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini leo Jumamosi Mei 13,2023.


Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Doris Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Old Shinyanga leo Mei 13,2023.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akizungumza na wanachama wa jumuiya ya wazazi kata ya Old Shinyanga leo Jumamosi Mei 13,2023.


Post a Comment

Previous Post Next Post