Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Taarifa kutoka kwenye chama cha waigizaji (TDFAA) Mkoa
wa Shinyanga
Msanii wa nyimbo za utamaduni katika kikundi cha Sanaa
Mkoani Shinyanga Arts Group, Bwana Fadhili Mungi jina maarufu Chap Chap anaomba
msaada wa matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua.
Msanii Chap Chap mwenye umri wa Miaka 44 ni mkazi wa
Msikamano kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga zaidi ya miezi miwili
akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa kutokwa na usaha puani, maumivu makali ya
kichwa , kutokwa na vipande vya nyama na maumivu mengine.
Taarifa hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa chama cha
waigizaji (TDFAA) Mkoa wa Shinyanga Neema Philipo Mushi ambapo amesema kwa mujibu
wa taarifa za madaktari anahitaji takribani shilingi Milioni Nne (4) ili aweze
kufanyiwa upasuaji ambapo kwa sasa anaendelea kutumia dawa za kutuliza maumivu
shilingi 98,000\= kila mwezi na kwamba miezi kadhaa amekuwa akiteseka.
Chap Chap anaiomba serikali pamoja na wadau mbalimbali
kujitokeza kumsaidia ilia pate matibabu kwani hana uwezo wa kifedha wa
kufanikisha matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua.
Chama cha waigizaji Mkoa wa Shinyanga kimeshaunda kamati
itakayoratibu na kupokea fedha kwa mtu anayeguswa Namba ya simu 0747956257 na
Mungu atakubariki.

Post a Comment