" POLISI TANZANIA, INTERPOL WAMKAMATA ALIYEWATAPELI WATALII

POLISI TANZANIA, INTERPOL WAMKAMATA ALIYEWATAPELI WATALII

 Polisi Tanzania, Interpol wamkata aliyewatapeli watalii


Jeshi la Polisi limesema limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyewatapeli watalii waliokuja nchini kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro, huku likibainisha kuwa Tanzania ni nchi salama kwa wageni wa ndani na nje ya Tanzania.


Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Maigwa,  katika lango la Mweka, ambalo hutumika kushuka kutoka katika Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu barani Afrika.


Ameongeza kuwa mtuhumiwa aliyekamatwa jina jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiupelezi, huku akibanisha kuwa mtuhumiwa  anatoka nje ya Tanzania, huku akiwaomba watalii hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania.


Kwa upande wake Bw. Chris Lomas ambae ni Mkurungenzi wa  kampuni ya hope for love, ameishukuru serikali na Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo wamelifuatilia swala hilo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliye watapeli. 

Post a Comment

Previous Post Next Post