" VIKUNDI VYA SUNGUSUNGU VYATAKIWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI ILI KUTOKOMEZA UHALIFU

VIKUNDI VYA SUNGUSUNGU VYATAKIWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI ILI KUTOKOMEZA UHALIFU


Vikundi mbalimbali vya Sungusungu kata ya Chambo Wilaya ya Ushetu Mkoani Shinyanga vimetakiwa kuendelea kushirikiana na wananchi pamoja na Jeshi la Polisi ili kufichua uhalifu na wahalifu kwenye maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa Januari 27, 2024 na mkaguzi Kata ya Chambo mkaguzi msaidizi wa Polisi Gwakisa Mwakalindile wakati alipokuwa anatoa elimu ya ulinzi shirikishi pamoja na ukamataji salama.

"Jeshi la Polisi linahakikisha ulinzi na Usalama salama kwa kila mwananchi lakini kumbuka ushirikiano wenu ni muhimu katika uhalifu na wahalifu katika maeneo yenu" alisema mkaguzi Mwakalindile.

Aidha, mkaguzi Mwakalindile alihitimisha kwa kuwataka wananchi wa Kata ya Chambo kutojichukulia Sheria mkononi bali kero zote zifikishwe kwenye vyombo husiku kwa ajili ya kupata suluhisho.

Kutoka Dawati la Habari Polisi Manispaa ya Shinyanga

 

Post a Comment

Previous Post Next Post