Na Mwandishi wetu, Misalaba Media - Tabora
JITIHADA za wadau wa elimu zinaendelea kuonekana hii ni kutokama na ajali ya kuungua moto kwa bweni la wanafunzi wa shule ya Sekondari Ziba iliyopo wilayani Igunga mkoani Tabora na kupelekea kuteketea kwa vitu vya wanafunzi wapatao 200 wanaosoma shuleni hapo, Tukio ambalo lilitokea Januari 23, 2024 katika moja ya bweni la wanafunzi wa shule ya Sekondari Ziba ambapo kwa sasa wadau mbalimbali wa elimu wameendelea kujitokeza kuisaidia shule hiyo.
Akieleza namna tukio lilivyotokea Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari Ziba Cassian Mbele amesema siku ya tukio hawakufanikiwa kuokoa chochote kutoka ndani ya bweni lililokuwa likiwaka moto.
"Tulipatwa na tukio la ajali ya kunguliwa na moja ya bweni la wavulana januari 23, 2024 majira ya saa 2 asubuhi ambapo wanafunzi wote walikuwa darasani, jambo la kumshukuru mungu hakuna mwanafunzi yoyote aliyedhurika zaidi ya uharibifu na wa vifaa vya wanafunzi na jengo" amesema Mbele.
Kwa upande wao wanafunzi waliokumbwa na janga hilo wameeleza namna hali ilivyokuwa baada ya tukio hilo na namna ajali hiyo alivyoathiri masomo yao huku wakilishukuru shirika la Luhende John Foundation kwa msaada wa masanduku ambayo yatawasaidia kuhifadhia misaada waliyopewa na wadau wa Elimu.
"Baada ya tukio hilo wanafunzi wote ilitubidi tuhamie kulala darasani kwa muda wa siku tatu na baadae tulihamishwa na kupelekwa kwenye bwalo la chakula ndipo tunapoishi mpaka sasa", wamesema wanafunzi.
"Tukio hilo lilipotokea tulikuwa darasani nguo zetu zote, vitabu, Madaftari vyote viliungua kwa moto hivyo ilituwia ugumi sana katika hali ya kujifunza". Wamesema wanafunzi.
Zoezi la utowaji wa misaada hiyo kwa wahanga wa tukio umeambatana pamoja na uzinduzi wa shirika la Luhende John foundation lenye makao makuu Mkoani Tabora ambapo katibu wa shirika hilo Abubakary Bukuku ameainisha malengo makuu ya shirika hilo lenye lengo la kusaidia jamii katika Nyanja ya Elimu, Michezo, Afya, uchumi pamoja na mazingira.
"Shirika la Luhende John foundation ni shirika lililoanzishwa mathubuti kwa ajili ya kusaidia wahitaji zaidi haswa katika nyanja ya Afya, Elimi, Michezo,, Uchimi pamoja na Mazingira kwa ngazi ya wilaya na Taifa kwa ujumla" Amesema Bukuku.
Awali akizindua shirika hilo lenye makao makuu wilaya ya Nzega katika Mkoa wa Tabora mwakilishi wa Mkuu wa wilaya hiyo afisa Tarafa Nyasa Ricardo Komanya amelitaka shirika kufanya kazi chini ya taratibu na sheria za nchi.
"Taasisi hii imeahidi kushirikiana na serikali hivyo ni matumaini yangu taasosi hii itasaidia jamii yetu, hatutakuwa tayari kushirikiana na taasisi ambazo hazifuati taratibu na sheria za nchi" Amesema Komanya.
![]() |
| Mwenyekiti wa Luhende John Foundation, John Luhendeakizungumza wakati wa uzinduzi wa shirika hilo. |
Mwenyekiti wa Luhende John Foundation akikabidhi Sanduku kwa mwakilishi wa wanafunzi pamoja na waalimi shule ya sekondari Ziba.

Post a Comment