" WASAFI MEDIA YAPEWA PONGEZI NA MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA

WASAFI MEDIA YAPEWA PONGEZI NA MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA

 Taasisi ya Wasafi Media imepokea cheti cha pongezi kutoka kwa mahakama kuu kanda ya Shinyanga kwa kuendelea kuhabarisha umma juu ya masuala ya mbalimbali ya sheria na mahakama nchini.


Pongezi hizo zimetolewa leo Februari 1, 2024 katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani humo kilichotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga na kupokelewa na mwakilishi na mwandishi wa Wasafi Media mkoani Shinyanga Abel Michael na kukabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga pamoja na Jaji Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Jaji Mfawidhi Frank Habibu Muhimbali.

Post a Comment

Previous Post Next Post