
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amewakumbusha Wakristo na hasa Wakatoliki kuendelea kubaki katika imani yao, hata pale wanapokutana na hali ya mateso.
Akiwahubiria mamia ya waamini ambao walihudhuria Misa ya mkesha wa Pasaka iliyofanyika katika Kanisa kuu la Mama mwenye huruma Ngokolo mjini Shinyanga, amebainisha kuwa, wapo baadhi ya wakristo ambo wamekuwa wakitoka katika imani yao na kwenda sehemu nyingine ambayo wanaamini watakwenda kuondolewa mateso yao jambo ambalo siyo la kweli.
Amewataka Wakristo wote kuendelea kusimama imara katika imani yao hata wakati wa mateso ambayo ni sehemu ya safari yao ya kumfuasa kristo na kwamba, imani yao imepatikana kwa njia ya mateso aliyoyapitia Kristo mwenyewe ili kumkomboa mwanadamu.
Amewataka kuacha maovu na kuendelea kuwa karibu na Mungu wakati wote kwa kutenda matendo mema .
Kupitia Misa hiyo ya mkesha wa Pasaka, Askofu Sangu amewabatiza wakatekumeni 34 pamoja na kutoa Sakramenti ya kipaimara kwa waimarishwa 57
Wakati huohuo amewataka watanzania kuendelea kusali kuombea amani, umoja, haki na mshikamano katika taifa ili viendelee kudumu

Askofu Sangu akiwa nje ya Kanisa kwa ajili ya Litrujia ya mwanga ambayo ni sehemu ya Misa ya Mkesha wa Pasaka

Askofu Sangu akijiandaa kuwasha mshumaa wa Pasaka






Askofu Sangu akichora alama ya Alfa na Omega katika mshumaa wa Pasaka

Askofu Sangu akiwasha mshumaa wa Pasaka


Maandamano kuingia Kanisani

Shemasi James Chingila akiwa amebeba mshumaa wa Pasaka

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akiwasha mshumaa

Wanakwaya wa Kwaya ya Watakatifu Malaika wakuu wakiimba kwenye Misa ya mkesha wa Pasaka


Walelewa wa Shirika la Kijimbo la Maria mtakatifu Mama wa huruma wakiwa kwenye Misa ya mkesha wa Pasaka

Wanakwaya
Bw. Peter Temu akisoma somo la kwanza

Shemasi James Chingila akisoma somo la Injili

Askofu Sangu akitoa homilia

Wabatizwa

Askofu Sangu akibariki maji kwa ajili ya ubatizo kushoto ni Paroko wa Parokia ya Ngokolo Padre Adolf Makandagu


Askofu Sangu akiwabatiza wakatekumeni




Waimarishwa


Askofu Sangu akitoa Sakramenti ya kipaimara



Askofu Sangu akiwanyunyizia maji ya Baraka waamini waliohudhuria Misa ya mkesha wa Pasaka



Post a Comment