" RATIBA YA MAZISHI YA HAYATI ALI HASSAN MWINYI

RATIBA YA MAZISHI YA HAYATI ALI HASSAN MWINYI





Hayati Rais Mstaafu Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi






TAARIFA KWA UMMA KUHUSU RATIBA YA MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAYATI ALHAJI ALI HASSAN MWINYI



Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;

Kama tulivyojulishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwamba Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, amefariki jana tarehe 29 Februari, 2024 saa 11.30 Jioni katika Hospitali ya Mzena,



kwa masikitiko makubwa, ninaomba kuungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa Salamu za Pole kwa Mheshimiwa Dr Hussein Ali Hassan Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, wanafamilia na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa wa kiongozi wetu mpendwa.



Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;

Kufuatia msiba huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza maombolezo ya siku saba na bendera kupeperushwa nusu mlingoti kuanzia leo tarehe 1 Machi, 2024. Katika kipindi hiki cha siku saba za maombolezo, Taifa litaungana kwa pamoja na wanafamilia katika maombolezo na mazishi ya Kitaifa yatakayofanyika huko Unguja Zanzibar kwa ratiba ifuatayo;.








1. Jumamosi tarehe 02 Machi, 2024;



i. Saa 12:00 Asubuhi;

Milango ya uwanja wa Amani itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi ambako Shughuli ya kitaifa itafanyika.



ii. Kuanzia Saa 3:00 Asubuhi;

Viongozi mbalimbali kuwasili uwanja wa Aman kwa ajili ya Maombolezo ya Kitaifa na Kuaga mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi



iii. Kuanzia Saa 4:00 Asubuhi;

Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi kuondoka nyumbani kwa marehemu kuelekea Uwanja wa Aman.



iv. Kuanzia Saa 5:00 Mchana;

Dua na swala kutoka kwa viongozi wa dini



v. Saa 5:30 Asubuhi

· Salamu za rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali

· Salamu za Pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



vi. Saa 6:30 Mchana

Viongozi na Wananchi mbalimbali kutoa heshima za mwisho



vii. Saa 9:00 Alasiri

Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi uwanja wa Aman kuelekea kijijini kwa marehemu Mangapwani kwa ajili ya mazishi ya Kitaifa



viii. Saa 10:00 Mchana

Wananchi na Viongozi mbalimbali kushiriki Mazishi ya Kitaifa ya hayati Ali Hassan Mwinyi eneo la Mangapwani.



Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;

Watanzania tumepokea taarifa za msiba wa mzee wetu, kiongozi wetu Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa masikitiko makubwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametutaka Watanzania wote kuwa watulivu na wastahimilivu kutokana na kifo cha mpendwa wetu.



Ndugu Wananchi na watanzania wenzangu; pamoja na taarifa hii, Serikali itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu matukio ya kila hatua kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali.





SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA

Post a Comment

Previous Post Next Post