
Na Mapuli Kitina Misalaba
Baadhi ya viongozi wa kampeni ya kupinga ukatili
Nchini SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga leo wamekutana na kuzungumza na Mkurugenzi wa
Shirika la Thubutu Africa Initiatives Bwana Jonathan Kifunda Manyama.
Viongozi hao pamoja na mambo mengine kwa pamoja
wameazimia kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao hasa ya
kupambana na vitendo vya ukatili huku Mkurugenzi Bwana Manyama akiipongeza
kampeni hiyo ya SMAUJATA kwa namna viongozi wanavyojitoa katika kuibua vitendo
vya ukatili.
Bwana Jonathan Manyama pia ni Mwenyekit wa mtandao
wa kupinga na kuzuia vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto Mkoa wa Shinyanga
( SHY-EVAWC)
Thubutu Africa Initiatives ni Shirika lisilo la
kiserikali linalotekeleza miradi katika maeneo matano (5) ambayo ni AFYA,
ELIMU, HAKI ZA BINADAMU, MAZINGIRA na MASHIRIKIANO na Taasisi zingine.
Shirika hilo ambalo linatakribani Miaka kumi
linatekeleza miradi katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini ikiwemo Mkoa wa Mwanza, Shinyanga, Tabora, Morogoro pamoja na Njombe.
Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga ambao
wameshiriki kikao hicho leo ni katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana
Daniel Kapaya, Mwenyekiti idara ya jinsia SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Inspekta Alkwin
Willa pamoja na Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Kishapu Bwana Emmanuel Makolo.
Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania
(SMAUJATA) ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini ambayo ipo Mikoa yote inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya
Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.
Kauli mbiu ya kampeni hiyo inasema “KATAA UKATILI
WEWE NI SHUJAA”

Baadhi ya viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wakiwa
kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa shirika la Thubutu Africa Initiatives Bwana
Manyama leo Machi 27,2024.

Baadhi ya viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wakiwa
kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa shirika la Thubutu Africa Initiatives Bwana
Manyama leo Machi 27,2024.
Post a Comment