
Afisa Mahusiano na Masoko wa Redio Faraja Bi.Getruda Thomas Muyonga, kesho Jumamosi tarehe 20.04.2024, atafunga Ndoa takatifu na Bw. Clement Madinda ambaye ni Mkaguzi msaidizi wa Madini mkoa wa Kimadini chunya mkoani Mbeya.
Bw. Clement Madinda pia alikuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM) mkoa wa Shinyanga, kabla ya kuhamia Chunya mkoani Mbeya.
Misa ya ndoa itafanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Stephano shahidi Parokia ya Nyasubi mjini Kahama, ambayo itaanza saa 4:00 asubuhi.
Getruda anakuwa ni mtumishi wa sita wa Redio Faraja kufunga ndoa katika miaka ya karibuni, akitanguliwa na watumishi wengine watano.
Misa ya ndoa na matukio mengine vitarushwa mubashara (Live) kupitia ukurasa wa Face book wa Redio Faraja, unaopatikana kwa anuani ya Radiofarajatz.
Post a Comment