" DC MHE. MHITA ATOA SIKU 7 KWA KAIMU MWENYEKITI WA MTAA WA SHUNU KUREJESHA FEDHA ALIZOPOKEA

DC MHE. MHITA ATOA SIKU 7 KWA KAIMU MWENYEKITI WA MTAA WA SHUNU KUREJESHA FEDHA ALIZOPOKEA


Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akitoa maagizo.


Na Sebastian Mnakaya, Kahama
MKUU wa wilaya ya Kahama MBONI MHITA ametoa siku saba kwa Kaimu mwenyeikiti wa serikali ya mtaa wa shunu JULIAS SABUNI kurejesha fedha kiasi cha shilingi laki tano na nusu alizopokea baada ya kuuza kiwanja katika eneo la bwawa la maji kwa MAIKO MASANJA huku akijua eneo hilo ni mali ya serikali.

Kauli hiyo imetolewa na MHITA katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika mtaa wa shunu kata ya Nyahanga Halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, ambapo amesema kuwa ofisi za serikali zisiwe sehemu za changamoto na badala yake ziwe za kutatua changamoto za wananchi zinazowakabili.
"Mzee wangu tafadhali sana naomba fedha ya huyu bwana arejeshewe, polisi kata natoa siku saba na jambo hili nakukabidhi ulifatilie na fedha ipatikane na kurejeshwa kwa muhusika" alimesema Mhiata.

MAIKO MASANJA, mkazi wa mtaa wa shunu akitoa kero yake katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Kahama MHITA amesema kuwa mwenyekiti huyo ameuza kiwanja hicho, huku baada ya siku kadhaa akiondolewa katika eneo hilo hali iliyomlazimu kuomba serikali ya mtaa kurudishiwa gharama zake alizonunua eneo hilo.

"Kero yangu kubwa mh mkuu wa wilayani ni kwamba eneo nilonunua kwa mwenyekita wa mtaa wa Shunu, naomba kwa sasa nihame na Kuna gharama nimetumia naomba unisaidia japo kurejeshewa fedha zangu kiasi cha shilingi laki tano na nusu" alisema Maiko Masanja

Akitoa ufafanuzi juu ya uzwaji wa eneo hilo, kaimu mwenyekiti wa mtaa wa Shunu JULIAS SABUNI amesema kuwa eneo hilo linamilikiwa na mama SALIMA ,ambapo tayari kiwanja hicho kina hukumu ya mahakama kuwa ni eneo lake halali, hali iliyosababisha kuhidhinishwa kuuzwa.

" niliuza eneo hilo baada ya kutambua kuwa ni la mama Salima ambaye ni mzanzibar  na kijana wake ndo aliliuza baada ya hukumu ya mahakama ni eneo lao na ndiyo maana nikahidhinisha saini ya mauziano" alisema Masabuni

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza.


Mkutano wa hadhara ukiendelea.


Mkutano wa hadhara ukiendelea.

Post a Comment

Previous Post Next Post