Na Elisha Petro
Klabu ya Chelsea inatarajia kuweka kambi nchini Marekani baada ya kumalizika kwa msimu huu 2023/2024 ili kujiweka sawa kuelekea msimu ujao 2024/2025.
24/07/2024 watacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Wrexham kutoka nchini Wales inayo shiriki league two nchini humo.
Baada ya siku tatu yaani 27/07/2024 watamenyana na Celtic mabingwa watetesi wanaoshiriki ligi kuu nchini Scotland na tarehe 31/07/2024 watashuka dimbani kuwakaribi América inayoshiriki ligi kuu nchini Mexico.
Mchezo wa nne kwa Chelsea atamkaribisha Manchester City 03/08/2024 na mnamo tarehe 06/08/2024 watamaliza michezo yao ya kirafiki dhidi ya Real Madrid.
Post a Comment