Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akizungumza kwenye baraza la madiwani la Halmashauri hiyo leo katika kikao cha pili mkutano wa robo ya tatu kwa Mwaka wa fedha 2023/2024.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga leo Mei 10, 2024 limeridhia hoja ya kufukuzwa kazi mtumishi mmoja kwa makosa mbalimbali ikiwemo utoro kazini zaidi
ya muda wa siku tano (5).
Mtumishi huyo anaitwa Msajigwa Julius Mwaipopo ambaye alikuwa idara
ya Ugavi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na kwamba alikuwa anatuhumiwa kwa
makosa mbalimbali ikiwemo utoro kazini.
Tamko la kufukuzwa kazi mtumishi huyo limetolewa kwa
niaba ya madiwani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe.
Ngassa Mboje
Azimio hilo la Madiwani, limefanyika baada ya
kuzingatiwa kwa taratibu zote za kisheria zinazotakiwa katika kuwawajibisha
watumishi wa Halmashauri.
“Tulikuwa
na shauri la kinidhamu moja leo la mtumishi mmoja na shauri hili kwa kauli moja
baraza la madiwani nimemfukuza kazi mtumishi mmoja ambaye anatoka idara ya
Ugavi jina anaitwa Msajigwa Mwaipopo kwahiyo haya yote tumeyafanya kwa pamoja
niwashukuru sana wajumbe kwa sababu haya yote yamejikita kwenye sheria na
taratibu zilizopo”.amesema Mhe. Ngassa Mboje
Wakati huo huo baraza la madiwani la Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga limewathibitisha rasmi kazini jumla ya watumishi 51.
Aidha katika mkutano wa Baraza hilo Madiwani pamoja
na viongozi wengine wamebainisha mambo mbalimbali ikiwemo changamoto za
miundombinu pamoja na Maji huku taarifa mbalimbali zikiwasilishwa.
Katika
taarifa yake kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Stewart Makali ameeleza kuwa ugonjwa wa
kipindupindu umeipuka na kuua watu wawili kata ya Mwakitolyo.
Amesema
Halmashauri hiyo ilipata wagonjwa 11 wa kipindupindu kati yao wawili wamefariki
dunia na kusema jitihadi mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na wataalam wa Afya
kwa kushirikiana na Halmashauri ili
kuthibiti ugonjwa huo.
“Halmashauri yetu imepokea taarifa
za uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu ambapo tarehe 30.4.2024 jumla ya watu kumi
na mmoja (11) waligundulika kuambukizwa ugonjwa huo katika kijiji cha
Nyaligongo kata ya Mwakitolyo, watu wawili walifariki”.
“Wagonjwa tisa (9) waliobaki
walipatiwa matibabu na kuruhusiwa na timu ya wataalam inaendelea kuwafuatilia,
Halmashauri imeshachukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huu kwa kugawa dawa za
kutibu maji kwa kaya 462, kutibu visima vya maji 16, kutoa elimu ya jinsi ya
kujikinga na maabukizi ya ugonjwa huu katika vitongoji vya namba moja, mbili na
namba tatu”.
“Natoa wito kwa jamii yote kuendelea
kuchukua tahadhari na kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu kwa
kuzingatia kutumia choo kikamilifu,
kunawa mikono kwa maji safi kabla na baada ya kufanya shughuli yoyote, usafi wa
mazingira, kula chakula kikiwa cha moto pamoja na kunywa maji yanayotoka kwenye
chanzo kinachoaminika na yawe yametibiwa”.amesema Makali
Misalaba
Media imezungumza na baadhi ya madiwani
ambao wameipongeza Halmashauri hiyo kwa jitihadi inazozifanya huku wakisisitiza
suala la usafi ili kuthibiti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo limefanya kikao cha pili katika Mkutano wa robo ya tatu kwa Mwaka wa fedha 2023/2024.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Stewart Makali akizungumza kwenye baraza la madiwani la Halmashauri
hiyo leo katika kikao cha pili mkutano
wa robo ya tatu kwa Mwaka wa fedha 2023/2024.
Baraza la
madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga likiendelea leo katika kikao cha
pili mkutano wa robo ya tatu kwa Mwaka wa fedha 2023/2024.
Baraza la
madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga likiendelea leo katika kikao cha
pili mkutano wa robo ya tatu kwa Mwaka wa fedha 2023/2024.
Baraza la
madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga likiendelea leo katika kikao cha
pili mkutano wa robo ya tatu kwa Mwaka wa fedha 2023/2024.
Baraza la
madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga likiendelea leo katika kikao cha
pili mkutano wa robo ya tatu kwa Mwaka wa fedha 2023/2024.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa idara, watendaji wa kata pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Shinyanga.

Post a Comment