Mgeni rasmi, Mkuu wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Paschal Shiluka akiwapongeza wanafunzi wa chuo hicho kwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi na wakunga Duniani.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto
Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga Mei 13,2024 wameadhimisha siku hiyo kwa
kutoa zawadi mbalimbali katika Hospitali ya Kolandoto ikiwa ni maadhimisho ya
siku ya wauguzi na wakunga Duniani ambapo huadhimishwa kila Mwaka ifikapo Mei
12.
Wanafunzi hao pamoja na mambo mengine wametembelea
na kutoa msaada katika Hospitali ya Kolandoto kama sehemu ya maadhimisho na
kumbukumbu ya siku ya wauguzi na wakunga Duniani.
Msaada huo ni Sabuni za unga, Sabuni za kipande
pamoja na Mafuta vimetolewa katika Wodi ya wazazi pamoja na chumba Cha wagonjwa
Hospitali ya Kolandoto.
Akizungumza katika hafla hiyo mkuu wa chuo cha
Sayansi za Afya Kolandoto Paschal Shiluka pamoja na mambo mengine amewapongeza wanafunzi
wa chuo hicho kwa kushiriki na kutambua umuhimu wa siku ya wauguzi na wakunga.
“Niwapongeza
sana kwa kuona umuhimu wa kuadhimisha siku hii na niwapongeza wanafunzi kwa
kutambua umuhimu wa kozi yenu kwamba
imeanzia wapi na sasa hivi tunaposherehekea matunda ya dada yetu Florence
Nightingate alikuwa mwanamke aliyechangia sana unesi wa kisasa, kwa ufupi tu
niwaambie taaluma ya uuguzi na ukunga niya kitaifa na kimataifa masomo yote
mnayoyasoma kwa sasa siyo tu ya kuishia hapa nchini hii ni mpaka kimataifa”.amesema
Shiluka
Mkuu wa idara ya uuguzi na ukunga katika chuo cha
Sayansi za Afya Kolandoto Mwalimu Wande
Kaeji ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza wanafunzi hasa wa kozi hiyo kuendeleza moyo wa majitoleo katika maeneo
mbalimbali bila kujali uwezo wa mtu.
“Mimi
nawaomba tu wanafunzi hawa ambao tunawafundisha na badae wataingia kutoa huduma
kwenye jamii nawaomba waendelee kutoa huduma kwa moyo wa upendo lakini pia kwa
kutokujali huyu ni maskini au ni tajiri na kawaida sisi wauguzi tunatoa huduma
zetu kwa moyo mmoja na kwakujitolea kwa sababu tunajua kazi ya uuguzi ni wito”.amesema
Mwalimu Wande
Katika risala ya wanafunzi wa kozi ya uuguzi na
ukunga chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto ambayo imesomwa na Shufaa Said
Tumkumbe amesema wameguswa kusherehekea siku ya wauguzi na wakunga Duniani kwa
kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kushiriki katika ibada ya maombi maalum,
kuona wagongwa kwenye wodi katika Hospitali ya Kolandoto na kuwapatia maadhi ya
mahitaji ikiwemo Sabuni na Mafuta.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Kolandoto Dkt.
Joseph Wallace Sahan amekishukuru chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kwa kutoa
msaada huo kwa wagonjwa.
“Nawashukuru
na kuwapongeza wauguzi wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya kwa namna ambavyo
wameendelea kuifanya kazi ya uuguzi katika Hospiatali yetu bega kwa bega pamoja
na sisi lakini pia uongozi nawashukuru sana kwa zawadi mbalimbali ambazo
wamezitoa siku ya leo kwa wagonjwa ambao wako mawondini zawadi hizi si chochote
lakini zinaleta faraja na kuonyesha tu kwamba ishara ya upendo kwa wagonjwa
ambao tunawahudumia na kwa hivyo inaleta faraja pia kwao tuko pamoja nao katika
maumivu ambayo wanayoyapitia”.amesema Dkt. Sahan
Maadhimisho ya siku ya wauguzi na wakunga Duniani yameongozwa na kauli mbiu inayosema “Muuguzi sauti ya kuongoza wekeza katika uuguzi na heshimu haki za kupata afya ya kimataifa”.
Muuguzi ni mtaalam wa afya aliyeandaliwa kupitia mfumo maalum na thabiti wa kitaaluma kisha kuthibitishwa na kuidhinishwa (na mamlaka iliyopo kisheria au chombo kinachosimamia taaluma hiyo) kutoa huduma za afya.
Wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto
Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga wakiwa katika maandamano ya amani kwenda
kuwaona wagonjwa wodini na kuwapa zawadi mbalimbali kwenye Hospitali ya
Kolandoto.
Wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto
Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga wakiwa katika zoezi la kukabidhi zawadi
mbalimbali katika wodi ya wazazi Hospitali ya Kolandoto.

mbalimbali katika chumba cha wagonjwa Hospitali ya Kolandoto.
Wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga wakiwa katika zoezi la kukabidhi zawadi mbalimbali katika chumba cha wagonjwa Hospitali ya Kolandoto.
Mkuu wa idara ya katika wodi ya wazazi Hospitali ya Kolandoto, Mariam Marco (katikati) akiwashukuru na kuwapongeza wanafunzi wa kozi ya uuguzi na ukunga chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kwa kuwatembelea na kutoa msaada.
Wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto
Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiwemo walimu
wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto baada ya maandamano leo Mei 13, 2024.

Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga wakiwa ukumbini kusherehekea siku ya wauguzi na
wakunga.
Wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto
Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga wakiwa ukumbini kusherehekea siku ya wauguzi na
wakunga.
Mkuu wa idara ya uuguzi na ukunga katika chuo cha
Sayansi za Afya Kolandoto Mwalimu Wande
Kaeji akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo amewashukuru wanafunzi huku akiwasisitiza kuendeleza moyo
huo wa majitoleo hasa katika jamii.
Mkuu wa idara ya uuguzi na ukunga katika chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Mwalimu Wande Kaeji akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo amewashukuru wanafunzi huku akiwasisitiza kuendeleza moyo huo wa majitoleo hasa katika jamii.
Mkuu wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Paschal
Shiluka akizungumza ambapo amesema chuo hicho kitaendelea kutatua changamoto
zinazowakabili wanafunzi hasa wa kozi ya uuguzi na ukunga ili kuwaimarisha
wanafunzi.
Mwanafunzi wa kozi ya uuguzi na ukunga chuo cha
Sayansi za Afya Kolandoto Shufaa Said Tumkumbe akisoma risala kwa niaba ya
wanafunzi wengine.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya
Kolandoto Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga wakiwa katika zoezi la kuonyesha kwa vitendo huduma
zinazofanyika katika wodi ya wazazi.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya
Kolandoto Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga wakiwa katika zoezi la kuonyesha kwa vitendo huduma
zinazofanyika katika wodi ya wazazi.
Mgeni rasmi, Mkuu wa chuo cha Sayansi za Afya
Kolandoto Paschal Shiluka akikabidhi zawadi iliyoandaliwa na wanafunzi wa kozi
ya uunguzi na ukunga kwa Mkuu wa idara ya uuguzi na ukunga katika chuo cha Sayansi
za Afya Kolandoto Mwalimu Wande Kaeji.
Mkuu wa idara ya uuguzi na ukunga katika chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Mwalimu Wande Kaeji akiwashukuru wanafunzi kwa kumpatia zawadi.

Post a Comment