Daktari mfawidhi wa Hospitali ya
Manispaa ya Shinyanga Moshi Lyobaa akitaja huduma za Afya zinazopatikana katika
Hospitali hiyo huku akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma bora.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Daktari mfawidhi wa Hospitali ya
Manispaa ya Shinyanga Moshi Lyobaa amewaomba wakazi wa Mkoa wa Shinyanga
kujitokeza kwa wingi kupata huduma mbalimbali za magonjwa ya nje na magonjwa ya
ndani katika Hostitali hiyo.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na Misalaba
Media ambapo amesema kwa sasa Hospitali
hiyo inatoa huduma zote kwa wananchi ikiwemo huduma ya meno, huduma ya matibabu
kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI, Huduma za matibabu kwa
wajawazito na watoto wachanga pamoja na huduma za matibabu ya dharura.
Amewaomba wananchi kujitokeza ili kupata
huduma kwa uharaka huku akiishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais
Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya uboreshaji wa majengo pamoja na vifaa vya
kutolea huduma katika Hospitali hiyo ya Manispaa ya Shinyanga.
“Katika
Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga huduma zipo na zinaendelea kuna huduma za
magonjwa ya nje, kuna huduma za magonjwa ya ndani, kuna huduma za matibabu kwa wajawazito na watoto wachanga, kuna
huduma za upasuaji kwa wa mama wajawazito, kuna huduma za Mionzi tunavifaa vya
kisasa kwa kweli tunamshukuru sana Rais Samia kwa sababu ametuwezesha kupata
vifaa vya kisasa ambavyo vinatuwezesha na kuturahisishia kazi zetu”.
“Lakini
pia tunahuduma ya Meno kuna mashine ya kisasa ya kung’olea Meno ambayo tumeipata
hivi karibuni tunaomba sana wagonjwa watu wote wenye changamoto waje kupata
huduma kwa sababu mashine ipo na niya kisasa zaidi huduma zingine tunazozitoa
ni huduma ya Macho, huduma za matibabu ya dharura yaani kwa wale ambao
wanahitaji huduma ya dharura kwa ukaribu naya haraka kuna madaktari wakutosha
na manesi wakutosha wenye uzoefu kwahiyo hizo huduma zote zinapatikana hapa
kwenye Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga”.
“Pia
tunahuduma za Maabara tunapima na tunamashine za kisasa zote zinafanya uchunguzi
wa magonjwa yote tunahuduma pia ya matibabu kwa watu wanaoishi na maambukizi ya
virusi vya UKIMWI pia tunahuduma ya baba mama na mtoto yaani tunahudumia kwa
kupima wajawazito, kupima watoto wadogo chini ya Miaka mitano pamoja na chanjo”.
“Tuna
Magari mawili ya Ambulance ambayo hata kama kuna changamoto wagonjwa tunaweza
kuwasafirisha haraka kuwapeleka katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa na ni bure labda
niseme kwamba kwa taratibu za huduma za Afya huduma huwa zinapatikana masaa 24
siku saba (Jumatatu hadi Jumapili) kwa maana ya kwanza Hospitali huwa haifungwi
muda wote tunatoa huduma masaa yote 24 changamoto ilikuwa ni kwamba watu
walikuwa wakipita wakiona ukarabati wanaona kwamba hii Hospitali haipo lakini
niseme kwamba Hospitali ipo na huduma zote zinapatikana hapa japo kuwa mnaona
tunaendelea na ukarabati lakini ni kuboresha tu maeneo ya kufanyia kazi lakini
huduma zote zipo zinaendelea kwahiyo watu wote karibuni sana kupata huduma na
ukizingatia hapa ni mjini katikati”.amesema Daktari Moshi
Mratibu wa huduma za kinywa na Meno
katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Anna Mwakapila amesema huduma ya
kinywa na meno kwa sasa inapatikana muda wote baada ya kupokea vifaa vya kisasa
kutoka serikalini.
“Huduma
zetu niza kisasa kwanza tumepata kiti kizuri chenye asesor zote unaweza
ukaziba Jino kwa dawa ya muda mfupi, unaweza ukaziba Jino kwa dawa ya muda mrefu,
unaweza ukatibu mzizi wa jino, unaweza ukaondoa kiini cha Jino lakini pia kung’oa
Jino lililoharibika vibaya hii ni hatua ya mwisho kabisa wananchi
tunawakaribisha mjitokeze kwa wingi kupata huduma hii wataalam wapo ni wa
kisasa wenye uzoefu, tunamshukuru Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kuweze
kufanikisha hii huduma”.amesema Mwakapila
Kwa upande wake mtaalam wa Mionzi katika
Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Evelyne Emmanuel ameeleza upatikanaji wa
huduma za Mionzi katika Hospitali hiyo huku akiwaomba wananchi kujitokeza.
Daktari mfawidhi wa Hospitali ya
Manispaa ya Shinyanga Moshi Lyobaa akitaja huduma za Afya zinazopatikana katika
Hospitali hiyo huku akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma bora.
Mratibu elimu ya Afya kwa umma Manispaa ya Shinyanga Salmon Mkanula akionyesha vifaa vya kisasa katika chumba cha kutolea huduma ya kinywa na Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mratibu elimu ya Afya kwa umma Manispaa ya Shinyanga Salmon Mkanula akiwakaribisha wakazi wa Shinyanga wanaosumbuliwa na Meno kwenda kupata huduma bora kwenye Hospitali hiyo ya Manispaa ya Shinyanga
Mratibu wa huduma za kinywa na Meno
katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Anna Mwakapila akionesha vifaa vya
kisasa vya kutolea huduma ya Meno katika Hospitali hiyo.
Mtaalam wa Mionzi katika
Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Evelyne Emmanuel akionyesha mashine ya ULTRASAOUND.
Mtaalam wa Mionzi katika Hospitali ya
Manispaa ya Shinyanga Evelyne Emmanuel akionyesha mashine ya ya kisasa ya X RAY.
Mtaalam wa Mionzi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Evelyne Emmanuel akionyesha mashine ya ya kisasa ya X RAY.
Vifaa vya kisasa katika chumba cha kutulea huduma ya Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Vifaa vya kisasa katika chumba cha kutulea huduma ya Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Vifaa vya kisasa katika chumba cha kutulea huduma ya Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Vifaa vya kisasa katika chumba cha kutulea huduma ya Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
TAZAMA VIDEO

Post a Comment