WATANZANIA wametakiwa kutanguliza misingi ya uzalendo na upendo katika jamii yetu Ili kuondoa tofauti miongoni mwetu ambazo zinachochea matabaka ya watu hapa nchini na kuvunja umoja wetu uliodumu kwa muda mrefu.
Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha viongozi wa Umoja wa Wazalendo Mkoani Mwanza Leo Jijini Mwanza, Kiongozi Mkuu na Mwenyekiti wa Wazalendo Mkoani Mwanza Bujiku Jackson aliwataka Watanzania kufuata yale yote mazuri ambayo yanaendeleza utamadunu wetu.
"Msingi Mkuu wa uzalendo ni umoja na maarifa hivyo ni wajibu wetu kuwezesha Watanzania kuyapa kipaumbele haya yote yenye tija katika shughuli za kila siku" alisema Jackson.
Alisema kuwa mmomonyoko wa maadili kwenye jamii yetu unaendelea kuchangiwa na kuingiliana kwa tamaduni zetu na zile za nchi za nje kwa kufanya watanzania kuiga utamaduni wa kigeni.
Naye Katibu wa Mahusiano ya Jamii na Umma wa Umoja wa Wazalendo Mkoani Mwanza Zuhura Mohamed alisema jamii katika ngazi mbalimbali inawategemea katika kuwaimarishia misingi ya upendo miongoni mwao ikiwa ni pamoja na kupenda vitu vyao wanavyozalisha na kutengeneza wenyewe.










Post a Comment