" SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA MADHEHEBU YA DINI-MAJALIWA

Facebook SDK

  • Tangaza nasi leo
  • Home
  • Contact us
  • About us
MISALABA  MEDIA - Habari kwa Maslahi ya Umma
  • Home
  • MAGAZETI
  • AFYA
  • MICHEZO
  • MATUKIO
  • MAKALA
  • AJIRA
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • SHINYANGA
  • HABARI

Top News

  • MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 14, 2025

  • MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 18, 2025

  • MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 15, 2025

  • MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 16, 2025

  • MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 17, 2025

  • DR. SAMIA - KATAMBI DAY YAZAA NEEMA KWA WANANCHI WA SHINYANGA KATAMBI ATOA MAMILIONI KILA KATA KUCHOCHEA MAENDELEO

  • MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 13, 2025

  • SMS za Kubembeleza Mpenzi Wako Au Mke

  • SHIRIKA LA HELPAGE TANZANIA LAENDESHA MAJADILIANO YA MAKUNDI RIKA WILAYANI KISHAPU KWA LENGO LA KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA NA MILA POTOFU

  • GOLD FM CHAMPIONS LEAGUE YAZIDI KUPAMBA MOTO, TIMU ZILIZOPITA KWENYE MCHUANO

HomeDINI

SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA MADHEHEBU YA DINI-MAJALIWA

Misalaba Media May 26, 2024 0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuthamini, kutambua na kuheshimu mchango wa madhehebu ya dini katika kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali nchini.

Amesema kuwa Serikali imekuwa ikishirikiana na Sekta binafsi zikiwemo Taasisi za dini katika kutoa huduma kwa wananchi na kuleta maendeleo ya Taifa kwa kuwa maendeleo ya nchi hayawezi kuimarika bila ushirikiano na ushirikishwaji wa kila mtu.

Amesema hayo leo (Jumapili Mei 26, 2024) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ibada ya kuwekwa wakfu kwa askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki Mbeya Mshashamu Godfrey Jackson Mwasekaga na Jubilei ya Miaka 125 ya Uinjilishaji jimbo kuu la Mbeya, iliyofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Cardinali Pengo.

“Ni ukweli usiopingika uwepo wa Taasisi za Dini unasaidia katika kuchangia juhudi za Serikali katika kutoa huduma mbalimbali kama vile elimu, afya, kilimo, maji na fedha, huduma ambazo Serikali peke yake isingeweza kuzifikisha kwa wananchi mara moja”.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inalipongeza kanisa Katoliki kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye kuimarisha utoaji na upatikanaji wa huduma bora za jamii kwa Watanzania.

“Hapa Mbeya na Mkoani Songwe ninafahamu kuwa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya linashirikiana na Serikali katika kutoa huduma afya katika maeneo 15 ya kutolea huduma ikiwemo Hospitali mbili za Igogwe iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na Mwambani iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, Vituo vya Afya vitatu (viwili Mkoa wa Mbeya na kimoja Mkoa wa Songwe); Zahanati 10 (7 zipo Mkoa wa Mbeya na 3 Mkoa wa Songwe)”

Pia, amewakikishia viongozi wa dini kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na madhehebu yote ya dini pamoja na wadau wote katika kuhakikisha huduma bora za afya na elimu hapa nchini zinapatikana

Kadhalika Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi wa dini waendelee kuweka msisitizo katika masuala ya kuwekeza katika vijana na kukemea vitendo vyote hatarishi kwa vijana mfano matumizi ya dawa za kulevya, wizi, ubakaji na kadhalika.

Amesema Serikali inatambua na kuthamini kazi na majukumu makubwa ya viongozi wa madhehebu ya dini ya kuwaongoza watu kiroho kwa kuwapa mafundisho, kutoa ushauri na kuwajenga kiimani.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Gervas Nyaisonga amesema kuwa Kanisa linatambua mchango mkubwa wa Serikali na kuunga mkono mipango ya maendeleo katika utoaji huduma za maji, umeme, barabara, afya na maeneo mengine.

“Kanisa linatoa pongezi kwa Serikali kwa utekelezaji wa programu mbalimbali za kumpunguzia mwananchi changamoto za kiuchumi na jamii”.

Kadhalika Askofu Mkuu Nyaisonga ameipongeza Serikali kwa kupinga vitendo vya ushoga na usagaji “endeleeni msimamo huo, kanisa lina msimamo imara wa kupinga vitendo hivyo”.










Tags DINI
  • Share

You Might Like

View all

Post a Comment

Post a Comment

Previous Post Next Post

EAST AFRICAN SPIRITS

 

Ubora wa East African Spirits (T) Ltd

 

HELLO TANZANIA!

Karibu MISALABA MEDIA, tunajihusisha na uchakataji na usambazaji wa habari na matukio mbalimbali mitandaoni, tukiwaletea taarifa zenye uhakika na uhalisia.

Huduma zetu zinaangazia:

  • Mikutano ya Hadhara: Matangazo ya moja kwa moja na kufuatilia mikutano na matukio muhimu ya kijamii na kisiasa.
  • Maafa na Majanga: Habari za haraka na taarifa za kina kuhusu majanga yanayotokea.
  • Habari za Ukatili, Burudani, na Michezo: Tunawaletea habari za kina, makala, na mahojiano ya kipekee kuhusu ukatili, burudani, na michezo.

KWETU NDIO MAHALA SAHIHI!

Pia tunatoa huduma za:

  • Video shooting za Nyimbo: Tunarekodi na kuchakata video za muziki kwa ubora wa hali ya juu.
  • Short clips na Short films: Tunatengeneza na kuchakata vipande fupi vya video na filamu za ubunifu kwa ajili ya matangazo, mitandao ya kijamii, na zaidi.

Kwa nini utuchague?

  • Uzoefu na Ubunifu: Timu yetu ya wataalamu ina uzoefu wa miaka mingi katika sekta ya habari na uchapishaji wa maudhui.
  • Ubora na Uaminifu: Tunajivunia kutoa huduma bora na za kuaminika kwa wateja wetu.
  • Upatikanaji: Tupo mtandaoni muda wote, tukihakikisha unapata taarifa muhimu kwa wakati.

Tembelea tovuti yetu: www.misalabamedia.com

Au tembelea mitandao yetu ya kijamii: YouTube, Instagram, Facebook, na X

Kwa maelezo zaidi au kuanza kushirikiana nasi, tupigie simu: 0745 594 231

HANSON'S CHOICE LADHA HALISI


Unapofurahia kinywaji chenye ladha halisi, unajivunia asili yako! Hanson's Choice – imeundwa kwa ubora, ladha murua, na fahari ya Tanzania.

Chagua kilicho bora kwa mlo wako wa jioni au sherehe maalum! 🥃✨

Nunua sasa na ujisikie tofauti!

📧 info@eastafricanspirits.com
📞 +255767650806 | +255652096254

Map Mastar MKM - Kataa Ukatili (Official Music Video)

January 05, 2023

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 6,2023

January 05, 2023

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

January 05, 2023

MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2024

January 04, 2025

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA JESHI LA POLISI

March 20, 2025

TAZAMA HAPA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI 2023

January 07, 2024

MKE WA BALTASAR WA VIDEO 400 ZA NGONO ,VIDEO YAKE YANASWA NA MUME MWINGINE

November 09, 2024

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2024

May 30, 2024

WANAFUNZI WALIOFUTIWA MATOKEO KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE 2023, TAZAMA HAPA

January 07, 2024

TANGAZO LA NAFASI 8, 000 ZA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KATIKA FANI MBALIMBALI

January 31, 2025

HANSON'S


GOLDBERG

 

Subscribe Us

CATEGORIES

  • AFYA
  • AJIRA
  • BIASHARA
  • BUNGENI
  • BURUDANI
  • DINI
  • EAST AFRICAN SPIRITS
  • ELIMU
  • HABARI
  • HISTORIA NA UTAMADUNI
  • IA
  • JAMII
  • Kilimo
  • KIMATAIFA
  • KITAIFA
  • MAGAZETI
  • MAKALA
  • MAP MASTAR
  • MATOKEO
  • MATUKIO
  • MICHEZO
  • MISALABA MEDIA
  • MUZIKI
  • POLISI
  • SHINYANGA
  • SHUWASA
  • SIASA
  • SIMULIZI
  • SMAUJATA
  • SONGS
  • TAARIFA
  • TANGAZO
  • TANZIA
  • UCHUMI
  • UKATILI
  • UTEUZI
  • VIDEO
  • WABUNGE MAJIMBONI
  • YouTube
  • ZANZIBAR

MISALABA MEDIA CHETI CHA PONGEZI

 

TUMESAJILIWA KUKUHABARISHA

MISALABA  MEDIA - Habari kwa Maslahi ya Umma

Most Popular

Map Mastar MKM - Kataa Ukatili (Official Music Video)

January 05, 2023

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 6,2023

January 05, 2023

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

January 05, 2023

MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2024

January 04, 2025

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA JESHI LA POLISI

March 20, 2025

TAZAMA HAPA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI 2023

January 07, 2024

MKE WA BALTASAR WA VIDEO 400 ZA NGONO ,VIDEO YAKE YANASWA NA MUME MWINGINE

November 09, 2024

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2024

May 30, 2024

WANAFUNZI WALIOFUTIWA MATOKEO KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE 2023, TAZAMA HAPA

January 07, 2024

TANGAZO LA NAFASI 8, 000 ZA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KATIKA FANI MBALIMBALI

January 31, 2025

TUMIA BIA YA BASEMBI

MISALABA MEDIA 2

 

NAMBA ZA KUPIGA SIMU POLISI

 

MISALABA MEDIA ALL RIGHTS RESERVED @2024 |
  • Home
  • About
  • Contact

Contact Form