HomeHABARI MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUKOMESHA UTORO KWA WANAFUNZI Misalaba July 29, 2024 0 Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaMsitahiki Meya wa Halimashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amewataka madiwani wote wa Halmashauri ya manispaa ya shinyanga kutokomeza utoro kwa wanafunzi kwa shule za Msingi na Sekondari.Mhe. Masumbuko ameyasema hayo leo Julai 29,2024 katika kikao cha baraza la madiwani kwa robo ya nne ya mwaka 2023/2024 cha kuwasilisha taarifa za utendaji kazi katika kata zao, ambapo amesema katika Manispaa ya Shinyanga bado utoro kwa wanafunzi ni mkubwa na kuwataka madiwani kusaidiana na maafisa Elimu Msingi na Sekondari ili kupunguza na kutokomeza utoro. "Watoto wengi hawaendi shule kwa sababu ya changamoto mbalimbali, sasa niwaombe waheshimiwa Madiwani twendeni tukasaidizane na maafisa elimu Msingi na Sekondari, tufanyeni jitihada za dhati kuhakikisha tunasaidiana kuondoa utoro kwa wanafunzi wetu kwani Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwisha boresha mazingira mazuri katika sekta ya elimu”. Amesema Mhe. MasumbukoKatika hatua nyingine madiwahi hao wamesema wanakabiliwa na changamoto za uhaba wa watendaji wa vijiji na mitaa ambapo wameiomba serikali kuwasaidia ili kupata watumishi hao. Akitoa ufafanuzi wa upungufu wa watumishi Mkuu wa Division ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Ndg. Pius Sayayi amesema Halmashauri ya manispaa ya shinyanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 imepata kibali cha kuajiri watumishi 151 katika nafasi mbalimbali ikiwemo Watendaji wa Vijiji na Mitaa. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza leo Julai 29,2024.Baraza la madiwani likiendelea katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.Diwani wa kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole akizungumza kwenye baraza hilo leo Julai 29,2024.Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze akizungumza kwenye baraza hilo leo Julai 29,2024.Bazara la madiwani likiendelea. You Might Like View all