Ticker

6/recent/ticker-posts

MADIWANI VITI MAALUM HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA WAMPONGEZA RAIS SAMIA NA MBUNGE WA JIMBO LA SOLWA MHE. AHMED SALUM

Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa CCM kata ya Lyamidati.

Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe. Zawadi Lufungulo Mwasha akizungumza kwenye mkutano  leo Julai 10,2024.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba  itapunguza au kumaliza kabisa changamoto za wananchi.

Wametoa pongezi hizo leo Jumatano Julai 10, 2024 kwenye ziara yao ya kutembelea kata za Halmashauri hiyo kwa lengo la kuhamasisha wanawake na wanachama wa CCM na jumuiya zake kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2024 pamoja na uchaguzi mkuu 2025.

Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameendelea na ziara yao ambapo leo wametembelea na kutoa elimu katika kata ya Lyabukande pamoja na kata ya Lyamidati.

Pamoja na mambo mengine wamempongeza Rais Samia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga  ambapo wamesema fedha zilizoletwa na Rais Samia zimetekeleza katika miradi mbalimbali kwenye sekta ya afya pamoja na elimu.

Pia wamempongeza Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum kwa maendeleo anayoyafanya katika Jimbo hilo.

Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe. Zawadi Lufungulo Mwasha amesema ipo miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa katika kata ya Lyabukande ikiwemo ujenzi wa madarasa pamoja na ujenzi wa Zahanati.

“Nimpongeze sana Rais wetu Mama Samia, amefanya mambo makubwa ya maendeleo kwa kipindi kifupi tu mabadiliko ni makubwa yaani ndani ya Miaka mitatu hakuna mtu aliyechangishwa michango kwenye ujenzi wa madarasa pia amekuwa akileta fedha za miradi mbalimbali za maendeleo kwahiyo tunampongeza sana lakini pia hata mbunge wetu wa jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum anasimamia jimbo letu vizuri sana tuendelee kumuombea sana mbele za Mungu maana tukipoteza hii bahati sijui kama tutakuja kuipata kwanza anaupendo na anahudumia wananchi wake bila upendeleo kwa sasa hapa Lyamidati kuna ujenzi unaendeleo wa jengo wa ofisi ya Chama cha kata ambayo ipo chini ya mheshimiwa mbunge kwahiyo niwaombe sana tuendelee kuwaunga mkono viongozi hawa”.amesema Mhe. Zawadi

“Kuna ukarabati wa madarasa ya shule ya msingi Lyabukande mradi huu fedha zimeletwa na Rais Samia mpaka sasa mradi huu umefikia hatua ya upakaji rangi na vigae, lakini pia kuna mradi wa ukarabati madarasa matatu kijiji cha Buzinza kata ya Lyabukande fedha za mradi zimeletwa na Mama Samia na mradi umefikia hatua ya upakaji rangi na vigae na alminiam”.

“Kuna ujenzi wa madarasa matatu shule ya sekondari Ahamed Kimandaguli kutoka fedha za jimbo ambapo mradi huu umefikia hatua ya usawa kufunga lenta, kuna ujenzi wa madarasa manne na ofisi moja hapa Lyabukande fedha zinatoka kwenye mfuko wa jimbo mradi huu umefikia hatua ya msingi tofari zipo”.

“Kuna mradi wa Umeme REA kwenye kijiji cha Lyagiti, Mapingili, Mwamakala na Buzinza fedha hizi zinatoka serikali kuu na mradi umefikia hatua ya ukamilishaji, lakini pia kuna mradi wa Maji ya ziwa unaendelea ambao gharama yake ni Bilioni 1.4”.

“Upo ujenzi wa Zahanati kijiji cha Mapingili ambapo boma tayari limekamilika, na kuna ujenzi pia wa Zahanati kijiji cha Mwashagi kwa nguvu ya wananchi mradi umefikia usawa wa msingi’.

“Miradi mingine inayoendelea ni ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Ng’wanangi, ujenzi wa choo cha mnada pamoja na ujenzi wa ofisi ya walimu Lyabukande sekondari kwahiyo niwaombe sana wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi na jumuiya zake tuendelea kuwaunga mkono viongozi wetu wote wanafanya vizuri wanajitahidi sana kuleta maendeleo kwenye maeneo yetu”.

Katibu wa madiwani  viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anastazia Robart Njile ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Tinde ameendelea kuwakumbusha wanawake na wanachama wa CCM na jumuiya zake kuwa kipaumbele wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura pamoja na daftari la makazi.

Katibu wa umoja  wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma  amewasisitiza wanawake wa UWT kujiamini na kuhakikisha wale wenye sifa wanachukua fomu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi  katika vijiji na vitongoji wakati utakapofika.

Pia amesisitiza wanachama kujisajili kwenye mfumo wa kielekroniki ili kuendelea kuwa wanachama imara wa Chama cha Mapinduzi CCM.

Kwa upande wake diwani wa viti maalum kata ya Tinde Mhe. Helena Daud Mwanambuli ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wanawake kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia unaoendelea kufanyika katika familia, jamii na maeneo mengine ili hatua zaidi za sheria ziweze kuchukuliwa kwa watuhumiwa.

Nao baadhi ya madiwani wengine wa viti maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameendelea kumpongeza mbunge wa jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum kwa kazi anazozifanya ambazo zinalenga kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

Pia wameendelea kuwakumbusha wanawake na wanachama wa CCM kuhakikisha wanakuwa kipaumbele katika hatua zote za uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika badae Mwaka huu 2024 pamoja na uchaguzi mkuu Mwaka 2025 ili waweze kumpigia kura mgombea wanayemhitaji kwa haki na amani.

Wamewaomba wananchi kuendelea kuwaunga mkono viongozi waliopo madarakani wakiwemo madiwani wa kata, mbunge wa jimbo la Solwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hasa katika shughuli za maendeleo.

Malengo ya ziara ya madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni kuhamasisha wanawake na wanachama wote wa CCM na jumuiya zake kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, kuhamasisha wanawake kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, Usajili wa wanachama wa CCM na jumuiya zake pamoja na na kukemea Ukatili wa kijinsia.

Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumatano Julai 10,2024 wametembelea kata ya Lyabukande yenye vijiji saba (7) ambavyo ni Mwamakasi, Lyabukande, Kimandaguli, Mapingili, Lyangili, Buzinza pamoja na Mwashagi.

Lakini pia wametembelea kata ya Lyamidati ambayo ina vijiji sita (6) ambavyo ni Ihagi, Kizungu, Mwabasa, Bukiligulu, Lyamidati pamoja na Kadoto.

Baadhi ya wanawake na wanachama wa CCM na jumuiya zake wamewapongeza madiwani wa viti maalum kwa kufanya ziara hiyo ambapo wameahidi kuzingatia yale yote ambayo wamekumbushwa iliwemo kuchua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe. Zawadi Lufungulo Mwasha akizungumza kwenye mkutano  leo Julai 10,2024 katika kata ya Lyabukande.

 

Madiwa wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga baada ya kuwasili katika kata ya Lyabukande.

Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe. Zawadi Lufungulo Mwasha akitoa zawadi kwa msanii ambaye ameimba wimbo maalum wa CCM.
Post a Comment

0 Comments