Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao amesema Jeshi la Polisi Mkoani humo limemuachia Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe kwa dhamana huku taratibu nyingine za kiuchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili zikiendelea.Akizungumza mchana huu, Kamanda Abwao amenukuliwa akisema “ameachiwa kwa dhamana ambayo imetolewa muda mfupi uliopita, anaweza kusafiri ( nje ya Mkoa wa Tabora) lakini atatakiwa kuja kuripoti tarehe aliyopangiwa ambayo ni tarehe 21 mwezi huu”
Asubuhi ya leo Kamanda Abwao akiongea na AyoTV alisema Jeshi la Polisi Tabora lilimkamata Ally Kamwe tangu jana usiku kwa mahojiano baada ya kutuhumiwa kutoa lugha chafu kwa Viongozi wa Serikali.

Post a Comment