" JWTZ YATANGAZA NAFASI ZA KAZI IKITOA ANGALIZO KWA MATAPELI

JWTZ YATANGAZA NAFASI ZA KAZI IKITOA ANGALIZO KWA MATAPELI





Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ ) Kanali Gaudentius Ilonda akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 30,2025 Jijini Dodoma wakati akitangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia elimu ya Sekondari hadi elimu ya juu.



Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ ) Kanali Gaudentius Ilonda,akisisitiza jambo Kwa waandishi wa habari leo Aprili 30,2025 Jijini Dodoma kuhusu nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia elimu ya Sekondari hadi elimu ya juu.

Na.Kulwa Meleka_Dodoma

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia elimu ya Sekondari hadi elimu ya juu.

Hayo yameelezwa leo April 30,2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ) Kanali Gaudentius Ilonda wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

Kanali Ilonda amesema sifa za mwombaji ni lazima awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na timamu,mwenye tabia na nidhamu nzuri,hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa, Cheti halisi Cha kuzaliwa(Original Birth Certificate)Vyeti vya Shule na taaluma.

Vilevile awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza,Chuo Cha Mafunzo au kikosi Cha kuzuia Magendo,awe amehitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT kwa mkataba wa kujitolea au mujibu wa sheria na kutunukiwa Cheti.

Amesema kwa vijana wenye elimu ya kidato cha Nne na kidato cha Sita wawe na umri usiozidi miaka 24,Vijana wenye Elimu ya Stashahada umri usiozidi miaka 26, Vijana wenye elimu ya juu umri usiozidi miaka 27,na Madaktari Bingwa wa binadamu umri usiozidi miaka 35 ya kuzaliwa

Aidha Taaluma adimu zinazohitajika ni Generall Surgeon,Orthopaedic Surgeon,Urologist Radiologist,ENT Specialist,Anaesthesiologist,Physician, Ophthalmologist, Paediatrician, Obstetrician & Gynaecologist,Ocologis, Pathologist, Psychiatrist, Emergency Medicine Specialist na Haematologist.

Pamoja na Medical Doctor, Dental Doctor, Veterinary Medicine,Bio Medical Engineer,Dental Laboratory Technician, Anaesthetic, Radiographer,Optometry, Physiotherapy na Aviation Doctor.

Aidha Taaluma za Uhandisi(Engineer) ni pamoja na Bachelor of Electronic Engineering, Bachelor of Mechanical Engineering, Bachelor in Marine Engineering, Bachelor in Marine transportation & Nautical Science, Bachelor in Mechanic in Marine Diesel Engine, Bachelor in Aviation Management, Bachelor in Aircraft Accident & Incident Investigation, Bachelor in Meteorology, Air Traffic Management & Aeronautic Engineering bila kusahau Fundi Mchundo Aluminum Welding na Welding & Metal Fabrication.

Sanjari na hayo utaratibu wa kutuma maombi kwa makundi yote mawili ni maombi yote yaandikwe Kwa mkono na yawasilishwe Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia Mei 1 2025 hadi tarehe 14 Mei,2025 yakiwa na Nakala ya kitambulisho cha Taifa au nambari ya NIDA,Nakala ya Cheti Cha kuzaliwa,vyeti vya Shule na chuo, Nakala ya Cheti Cha JKT kwa waombaji waliomaliza mkataba wa kujitolea pamoja na nambari ya simu ya mkononi ya Mwombaji.

Kuhusu miaka isiyozidi 35 kwa madaktari bingwa wa binadamu kuwa mdogo,Kanali Ilonda amesema wamefanya hivyo kutokana na kuwapa kipaumbele vijana na wamepima Kisayansi na kuona umri huo ni sahihi.

“Kule pia kuna mafunzo magumu ndio maana tuwepa Nafasi zaidi vijana lakini ukifuata mtiririko wa kuanzia shule ya msingi mpaka Chuo Kikuu bado miaka 35 ni michache kwani tuna madaktari bingwa wengi ambao wapo chini ya miaka 30,”amesema Kanali Ilonda.

Kuhusu kutoa nafasi zaidi katika kada ya afya kuliko kada zingine,Kaimu Mkurugenzi huyo wa Habari na Uhusiano JWTZ,amesema mahitaji yamekuwa makubwa kutokana na ongezeko la Hospitali za Jeshi.

“Tuna Lugalo,tuna Hospitali mpya Msalato ambayo itahudumia Askari na wananchi mahitaji ni makubwa ndio maana tumeipa msukumo mkubwa fani hiyo,”amesema Kanali Ilonda.

Hata hivyo ametoa angalizo kwa wananchi kutokubali kurubuniwa na matapeli kwa kudai hatua kali zitachukuliwa kwao ikiwemo kupelekwa Polisi.

“Naomba niwakumbushe hakuna nafasi ya kujiunga Jeshini kwa kutoa fedha atakae toa na kupokea Sheria ipo pale pale hatua Kali kwao zitachukuliwa,”amesema Kanali Ilonda

Post a Comment

Previous Post Next Post