Akizungumza na MISALABA MEDIA leo Mei 22, 2025, ofisini kwake, Bwaga amesema maandalizi ya kumpokea kiongozi huyo yamekamilika, na wanachama pamoja na wakazi wa Shinyanga wanakaribishwa kushiriki kwa wingi katika mkutano huo muhimu wa chama.
“Mkutano huu ni sehemu ya ziara ya kitaifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ambaye anapita katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kutoa elimu ya kisiasa kwa wanachama wa CCM,” amesema Bwaga.
Ameongeza kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Town kuanzia majira ya asubuhi, ambapo mbali na Makalla, viongozi wengine wa CCM ngazi ya mkoa na wilaya watahudhuria.
Aidha, Bwaga ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi ili kusikiliza maelekezo na mafunzo ya chama, pamoja na kutoa maoni yao kwa ajili ya kuimarisha ustawi wa jamii kupitia Ilani ya CCM.
MISALABA MEDIA itaendelea kukufahamisha kila kinachojiri kuhusu ujio huo wa kiongozi huyo wa kitaifa.
Post a Comment