Na Belnardo Costantine, MisalabaMedia
Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linamshikilia Joseph Muhulila (28) Mwendesha Bodaboda na Mkazi wa Mtaa wa Lukosi kata ya Mkwawa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Kwa tuhuma za mauaji Mtoto wake aliyejulikana kwa Timotheo Joseph Muhulila mwenye umri wa miaka 6 Kwa kumchinja na kutenganisha viungo vyake Kisha kutupa mabaki ya mwili kwenye shimo la Choo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Lukosi Kenedi mahona amesema ni wiki tatu zimepita tangu mzazi huyo alipotoa taarifa za kupotelewa amtoto wake,
baada uya upelelezi wa jeshi la polisi amekiri kuhusika kwenye mauaji hayo.
Hata hivyo Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji MelkSedeck Banzi amesema wametoa baadhi ya vipande vya nyama ambapo bado haijathibitishwa Moja Kwa Moja kama ni vipande vya Binadamu.
sambamba na hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi akithibitisha kutokea Kwa tukio hilo.
Post a Comment