Na Mwandishi wetu, Misalaba Media -Kagera
Evance Kamenge, mchumi na mkulima kutoka Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, ametoa shukrani zake kwa chama cha Mapinduzi (CCM) huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia uzinduzi rasmi wa Ilani ya utekelezaji ya CCM ya mwaka 2025 – 2030 kutokana na ilani hiyo yenye maono na matumaini makubwa.
Kamenge ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa Manispaa ya Bukoba, muda mfupi baada ya kuwasili mkoani Kagera akitokea Dodoma ulipofanyika uzinduzi rasmi wa ilani hiyo.
Kamenge ametilia mkazo umuhimu wa ilani hiyo na kuelezea kwamba ina maono yenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika uongozi.
"Nampongeza Rais Samia Mama mbeba maono nakipongeza chama changu chenye kuleta mabadiliko chanya hakika kitasonga mbele daima na kubeba fikra za wenye mapenzi nacho" alisema Kamenge.
Kamenge ni kijana mwenye uwezo wa kipekee katika masuala ya kisiasa, akijulikana kwa mtazamo wake wa kisasa na namna anavyoweza kuwasiliana na vijana na jamii kwa ujumla.
Kamenge amekuwa akijaribu kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia sera za maendeleo, ushirikiano, na uwajibikaji.
Amesema kuwa ilani hiyo inampa nguvu na kusababisha kumpa matarajio ya kuelekea kuunda jukwaa la kujihusisha na vijana ili kuwapa sauti katika maamuzi yanayowahusu, ikiwa ni pamoja na miradi ya kuendeleza uelewa wa kisiasa miongoni mwa vijana.
Mwanasiasa huyo pia amesema anatarajia kuleta mabadiliko katika sera za kiuchumi, kijamii, na kisiasa ili kuboresha maisha ya wananchi, hasa wale wa chini katika jamii.
Evance Kamenge anaweza kuwa kiongozi mwenye nguvu katika siku zijazo, akiwa na uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa na chanya katika siasa na maendeleo ya jamii.
Post a Comment