" ACT WAZALENDO YATISHIA KUISHTAKI SERIKALI, KUFUNGUA KESI IKIWA MITANDAO YA KIJAMII YA X, TELEGRAM NA CLUBHOUSE HAITAFUNGULIWA

ACT WAZALENDO YATISHIA KUISHTAKI SERIKALI, KUFUNGUA KESI IKIWA MITANDAO YA KIJAMII YA X, TELEGRAM NA CLUBHOUSE HAITAFUNGULIWA

 Chama cha ACT Wazalendo kimepinga vikali hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufunga mitandao ya kijamii ikiwemo X (zamani Twitter), Clubhouse na Telegram, kikisema hatua hiyo ni kuvunja katiba ya nchi, hasa ibara ya 18 inayotoa haki ya uhuru wa kutoa maoni na kupata taarifa.

Katika taarifa iliyotolewa leo Juni 25, 2025 na Naibu Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA kupitia ACT Wazalendo, Emmanuel Ntobi, chama hicho kimetishia kufungua kesi mahakamani endapo mitandao hiyo haitafunguliwa mara moja. Aidha, kimedai kuwa kufungwa kwa mitandao hiyo ni dalili za wazi za juhudi za serikali kuficha taarifa muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

ACT Wazalendo kimesisitiza kuwa mitandao hiyo ni chanzo muhimu cha upatikanaji wa habari kwa wananchi, na kuwa hatua ya kuifunga ni kuzuia wananchi kupata taarifa muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post