" MAAZIMIO YA SEMINA YA EWURA NA MISA-TAN YATOA MWELEKEO MPYA KWA WAANDISHI WA HABARI

MAAZIMIO YA SEMINA YA EWURA NA MISA-TAN YATOA MWELEKEO MPYA KWA WAANDISHI WA HABARI

Na Mapuli Kitina Misalaba
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika juhudi za kuwafikishia wananchi elimu juu ya wajibu wao na namna ya kunufaika na huduma za nishati na maji.

Kauli hiyo imetolewa leo Juni 16, 2025 na Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Nyirabu Musira, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu mamlaka hiyo na majukumu yake na kwamba semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Beachcomber Hotel, jijini Dar es Salaam.

Musira amesema ushirikiano kati ya EWURA na vyombo vya habari ni muhimu kwa kuwa waandishi ndio daraja la kuifikia jamii, hivyo ni vema wakaelewa kwa undani kazi na wajibu wa mamlaka hiyo ili waweze kuhabarisha kwa usahihi na kuelimisha wananchi.

Semina hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), ikiwa na lengo la kuwaimarisha wanachama wake katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MISA-TAN, Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa kushirikiana na taasisi hiyo, akieleza kuwa semina hiyo ni hatua muhimu ya kuimarisha mahusiano baina ya EWURA na vyombo vya habari.

Soko ameongeza kuwa, waandishi waliopata elimu hiyo wataweza kuandika habari zenye matokeo chanya na kusaidia kutatua changamoto za nishati na maji katika jamii.

Akizungumza wakati wa semina hiyo, Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma kutoka EWURA, Wilfred Mwakalosi, ameeleza kwa kina kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo pamoja na matarajio ya EWURA kwa waandishi wa habari katika kusaidia kuelimisha umma.

Naye Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, Alex Benson akisoma maazimio ya semina hiyo, amesema nimuhimu semina kama hiyo kuendelea kufanyika kwa wanachama wa MISA-TAN katika mikoa yote ili kuongeza uelewa kwa wanahabari kote nchini.

Makamu Mwenyekiti wa MISA-TAN Roda Marumo amewahimiza waandishi waliopata elimu hiyo kwenda kuwa mabalozi wazuri katika jamii, huku akiipongeza EWURA kwa kutoa mafunzo hayo muhimu kwa tasnia ya habari.

Semina hiyo imehudhuriwa na wanachama wa MISA-TAN kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Pwani, Dar es Salaam na Shinyanga, ambao wameahidi kutumia elimu waliyoipata kwa vitendo, huku wakipata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa na wataalamu kutoka EWURA.

Kwa pamoja, washiriki wameonesha ari ya kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika sekta ya nishati na maji kupitia kazi zao za uandishi wa habari.




Semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na majukumu yake inaendelea leo katika ukumbi wa mikutano wa Beachcomber Hotel, jijini Dar es Salaam.

Semina hiyo imefunguliwa rasmi na Nyirabu Musira kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, ambapo amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuelewa kazi na majukumu ya EWURA ili waweze kuhabarisha jamii kwa usahihi na ufasaha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa hiyo  hiyo, akisema kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano baina ya mamlaka hiyo na vyombo vya habari nchini.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ambao ni wanachama wa MISA-TAN kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Pwani, Dar es Salaam na Shinyanga, wameahidi kuzingatia yale wanayojifunza kupitia mawasilisho mbalimbali na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo katika kazi zao za kila siku za uandishi wa habari.

Semina hiyo inaendelea, ikilenga kuimarisha uelewa wa wanahabari juu ya mfumo wa udhibiti wa sekta ya nishati na maji nchini.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya Mashariki akifungua semina hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa EWURA leo Juni 16, 2025.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya Mashariki akifungua semina hiyo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa EWURA leo Juni 16, 2025.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko akitaja malengo ya semina hiyo leo Juni 16, 2025.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko akitaja malengo ya semina hiyo leo Juni 16, 2025.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko akizungumza kwenye semina hiyo leo Juni 16, 2025. 

Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma kutoka UWURA, Wilfred Mwakalosi akielezea EWURA na majukumu yake pamoja na matarajio ya EWURA kwa Waandishi.

Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma kutoka UWURA, Wilfred Mwakalosi akielezea EWURA na majukumu yake pamoja na matarajio ya EWURA kwa Waandishi.



 

Post a Comment

Previous Post Next Post