Na Elisha Petro, Misalaba Media
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na taasisi mbalimbali,wadau na jamii kwa ujumla kuendelea kutunza mazingira kwa kutoa Elimu juu ya umuhimu wa upandaji wa miti ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Shinyanga.
Naibu Waziri Khamis amesema kuwa hadi sasa, Serikali imeandaa mpango mkakati unaojumuisha sera na sheria za utunzaji wa mazingira, kwa lengo la kuhamasisha na kutekeleza shughuli za uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya taifa.
“Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha miti inapandwa kwa wingi, ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Tumeweka mkakati madhubuti unaolenga kuleta tija katika kulinda na kuhifadhi mazingira yetu,” alisema Mhe. Khamis.
Aidha, Naibu Waziri ametumia maadhimisho hayo kuwasihi wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuepuka shughuli zinazoathiri mazingira, ikiwemo ukataji miti holela na ufugaji usiozingatia utaratibu, akisisitiza kuwa hatua hizo zitasaidia kuwa na mazingira bora na endelevu.
“Tuendelee kupanda miti na kumtunza mazingira yetu natambua kuwa tunazo shughuli zetu za kilimo na ufungaji naomba shughuli hizo zisiathiri mazingira yetu kwani kwa hapa tulipofikia sio tena muda wa kukata miti lakini leo nimefurahi kwa kuwahimiza watoto wetu,viongozi wa dini na wazee wetu waliokusanyika hapa kwa ajili ya kupata Elimu ya upandaji wa miti tutambue kuwa ukataji wa miti ovyo na ufugaji holela wa mifugo ni changamoto kubwa tuzidi kudhibiti haya na tulifanya hivyo basi tutajenga mazingira bora kwa vizazi vya sasa na vijavyo,” amesema Naibu Waziri Khamis
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Julius Mtatiro, amesema kuwa mkoa wa Shinyanga umepiga hatua kubwa katika suala la uhifadhi wa mazingira ikilinganishwa na miaka ya nyuma na kuahidi kuwa uongozi wa mkoa huo utaendelea kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na taasisi binafsi ili kuimarisha zaidi juhudi utunzaji wa mazingira.
“Mkoa wa Shinyanga umeanza kuona matokeo chanya ya jitihada za utunzaji mazingira na nikuhakikishie Naibu Waziri kuwa wananchi I wa Shinyanga tutaendelea kushirkiana kwa pamoja katika kupanda miti na kuzidi kuelimishana kuhusu umuhimu wa miti kwani tunakumbuka kuwa i hii imekuwa Manispaa ya kwanza Tanzania kwa usafiri lakini kwa mwaka huu tumekuwa nafasi ya pili kwa Tanzania kwa hiyo tutazidi kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha tunalinda mazingira yetu kwa ajili ya maendeleo endelevu,” alisema Mhe. Mtatiro.



Post a Comment