" RWAMUTOGA AUTAKA UBUNGE MISSENYI AJA NA VIPAUMBELE KABAMBE

RWAMUTOGA AUTAKA UBUNGE MISSENYI AJA NA VIPAUMBELE KABAMBE


Na Mwandishi wetu, Misenyi

Burchard Rwamutoga, ni mjasiliamali na mchumi namsomi anayezaliwa katika kata ya Kasambya, Missenyi mkoani Kagera, ametangaza nia yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Missenyi.

 Rwamutoga amesisitiza kujitolea kwake kupambana kwa nguvu na maarifa katika kuleta maendeleo ya wana Missenyi huku akieleza kuwa atazingatia vipaumbele muhimu kama elimu na ajira, hasa kwa vijana.

Katika mazungumzo yake, na vyombo vya habari Rwamtoga amebainisha kuwa, endapo akipata ridhaa ya kuongoza atatumia ujuzi na maarifa aliyopata ili kusaidia jamii katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Majasiliamali  huyo amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni ufaulu usioridhisha ukisefu wa ajira kwa vijana, ambapo ameahidi kuwezesha vijana jimboni humo kujiajiri wenyewe.

Rwamutoga pia ameelezea historia yake ya kielimu, akisema kuwa alimaliza shule ya msingi Kasambya kisha akachaguliwa kujiunga na shule ya sekondari iliyoendeshwa na wakulima wa kahawa, ambapo alifanya vizuri licha ya changamoto za kifedha.

Amesema kuwa aliendelea kusoma masomo ya uchumi na hesabu katika shule ya sekondari ya serikali mkoani Dodoma na kupata nafasi ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kabla ya kujiunga na masomo ya juu.

Ameeleza kuwa baada ya kumaliza masomo yake, alifanya kazi katika wizara ya Fedha na alihitimu diploma ya uhasibu na baadaye alijikita katika kusaidia jamii zisizojiweza.

Ameongeza kuwa alisoma zaidi Nchini Uingereza na Nepal katika masuala ya utawala na maendeleo jumuishi, na pia kufanya kazi kama mkufunzi wa wakufunzi Nchini New Zealand.

Vile vile amesema ana maono ya dhati ya kuboresha maisha ya wana Missenyi kwa kutumia elimu na uzoefu wake katika maendeleo ya jamii.

Ameongeza kuwa miaka miwili baada ya kuchaguliwa, alisoma diploma ya juu ya uhasibu katika chuo cha usimamizi wa Fedha na  baada ya kumaliza masomo hayo, alijitahidi kusaidia kuinua familia zisizojiweza na baadaye alihitimu diploma nyingine katika chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo alisoma masuala ya fedha.

"Baada ya hapo, nilijiunga na shule ya kimataifa iitwayo Tanganyika, ambapo niliteuliwa kuwa msimamizi wa mradi wa utengamao kwa watu wenye ulemavu katika eneo la Rufiji"alisema Rwamtoga 

 Katika nafasi hiyo, alifanya kazi kwa zaidi ya miaka 13 kabla ya kujiunga na shirika la kimataifa la Ujerumani kama mratibu wa mradi wa maendeleo ya jamii na baada ya kupata uzoefu huo, alipata nafasi na mwaliko wa kuendeleza masomo yake zaidi.

Alifanya safari ya kwenda Uingereza, ambapo alisoma utawala na fedha Hatimaye, alisafiri hadi Nepal ili kujifunza kozi kuhusu maendeleo jumuishi kwenye jamii. 

Katika hatua nyingine ya maendeleo ya kitaaluma, alisafiri hadi New Zealand kuwa mkufunzi wa wakufunzi katika masuala ya maendeleo jumuishi katika jamii.

Amefafanua kuwa Ujuzi na uzoefu aliyoupata nchini New Zealand ulimwezesha kufanya kazi na Nchi mbalimbali zikiwemo Afghanistan, Nigeria, Ethiopia, na Liberia. 

Aidha ameeleza kuwa baada ya kurudi Tanzania, kufanya kazi kama mwakilishi mkaazi wa shirika hilo, ambapo alihusika katika miradi mbalimbali iliyosimamiwa na shirika hilo katika maeneo mbalimbali nchini.

Hivi sasa, Rwamtoga ni mjasiliamali na muelimishaji wa jamii katika masuala ya uboreshaji wa maendeleo kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja.

Amesema endapo atakuwa kiongozi katika nafasi ya  kuwa mbunge, atahakikisha atabadilisha mwangaza wa matumaini, hususan kwa vijana kwa upande wa ajira. 

Hata hivyo amesema kuwa katika utaratinj wake akakuwa anaitisha kikao cha wadau wa maendeleo walio ndani na nje ya jimbo la Missenyi ili kujadili changamoto zinazokabili jamii, kwa lengo la kuona njia za pamoja za kutatua matatizo hayo kila mwaka.


Post a Comment

Previous Post Next Post