" THOMAS MGONTO KITIMA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE IKUNGI MASHARIKI

THOMAS MGONTO KITIMA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE IKUNGI MASHARIKI

Aja na Kauli Mbiu: “Tukiinuliwa, Tutawainua Wengi” Na Mwandishi Wetu, Ikungi Kada na mwanaharakati kijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Thomas Mgonto Kitima, ameanza safari yake ya kisiasa kwa kishindo baada ya kuchukua rasmi fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki. Kitima, ambaye anafahamika kama kiongozi makini na mwenye dira ya maendeleo, amesema dhamira yake kuu ni kuhakikisha wananchi wa Ikungi Mashariki wananufaika na huduma bora za kijamii, hususan elimu, afya, maji safi na miundombinu ya kisasa. Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Kitima amewaomba wananchi wa Ikungi Mashariki kumpa ushirikiano katika kipindi hiki cha mchakato wa kisiasa, huku akiahidi kuendelea kuwa mtumishi wa kweli wa wananchi, sambamba na kauli mbiu yake: “Tukiinuliwa, Tutawainua Wengi.” Wananchi kadhaa wameeleza imani yao kwake, wakisema ni mtu sahihi wa kulipeleka jimbo hilo mbele kimaendeleo na kuimarisha umoja wa jamii, kwani jitihada zake za kusaidia zimekuwa zikionekana kwa muda mrefu. Kupitia taasisi yake isiyo ya kiserikali, Chifu Mgonto Foundation, Kitima amekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali, zikiwemo kilimo, elimu na uwezeshaji wa vijana na wanawake.

Post a Comment

Previous Post Next Post