" WAVUTIWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KIMKAKATI

WAVUTIWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KIMKAKATI

Baadhi ya wananchi wamepongeza juhudi zilizofanywa na serikali ya awamu sita kwa utekelezaji Mkubwa wa Miraji ya kimkakati ikiwemo kukamilika kwa Daraja la Kigongo Busisi hivi karibuni.  
 
Wito huo umetolewa kwa nyakati tofauti Jijini Mwanza na wadau wa maendeleo wakielezea kuona Miradi Mingi ikielekea kukamilika huku Daraja refu Barani Afrika lenye urefu wa zaidi ya kilomita 3  ukiwa
umekamilika.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoani Tabora Mhandisi Raphael Mulimaji alisema anavutiwa na kasi ya utekelezaji miradi ya maendeleo iliyofanyika tangia serikali ya awamu ya sita ianze.

Alitaja miradi ya kimkakati ambayo ina maslahi makubwa kwa taifa kuwa ni Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambalo tayari limeanza kuzalisha umeme na Trani ya Mwendokasi ya SGR ambayo imeanza kutoa huduma toka Dar es Salaam  hadi Dodoma Kuwa ni mafanikio ambayo watanzania wanafurahia.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post