Edwin Soko (TMFD)
Tanga
Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi kwenye sekta ya uvuvi yamekutana Jijini Tanga kuweka mikakati ya kufanya kazi Kwa kushirikiana baiana ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na mashirika hayo.
Mkutano huo umeratibiwa na Wizara ya mifugo na uvuvi Kwa kukutanisha mashirika ya yasiyo ya kiserikali mbalimbali.
Mkurugenzi wa Uvuvi Profesa. Prof. Mohammed Sheikh alisema kuwa, kikao hicho ni muhimu sana Kwa kuwa kinatoa fursa kwa Wizara kusikiliza wadau wanasema nini juu ya kazi zinazofanya na Wizara na nini changamoto za kisekta na namna gani ya kuzitatua.
Profesa Sheikh pia amewashukuru wawakilishe wote wa mashirika na kupata nafasi ya kuwapitisha kwenye vipaumbele vinne vya Wizara ya mifugo na uvuvi Tanzania.
Naye Mratibu wa mashirika ya yasiyo ya kiserikali toka dawati la uvuvi Tumaini Chambua alipata nafasi ya kuwapitisha washiriki kwenye mwongozo wa mashirikiano baina ya Wizara (sekta ya uvuvi)na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Mkutano huo ni wa siku mbili na umeshirikisha mashirika yasiyo na kiserikali ya ndani ya Nchi, kimataifa na Wizara ya mifugo na uvuvi.
Mkurugenzi wa Uvuvi Prof.Mohammed Sheikh akifungua kikao Kati ya Wizara ya mifugo na Uvuvi na Asasi zisizo na kiserikali
Post a Comment