" ZITTO Kabwe: Polisi Nitendeeni Haki Mimi Ndio Rais Ajaye

ZITTO Kabwe: Polisi Nitendeeni Haki Mimi Ndio Rais Ajaye

 

Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameonya vyombo vya dola, hasa polisi, dhidi ya kile alichokiita kutumiwa kisiasa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema kwamba mabadiliko ya uongozi ni jambo la kawaida katika demokrasia, na kwamba wale wanaowatendea wananchi visivyo leo, huenda wakakutana nao kama viongozi wa juu wa nchi kesho.

Akizungumza Julai 10, 2025 katika mkutano wa hadhara katika Jimbo la Tunduru Kaskazini mkoani Ruvuma, Zitto amesema kuwa vyombo vya usalama vinapaswa kujiandaa na mabadiliko ya uongozi, na kuacha kutekeleza maagizo ya kisiasa kwa upendeleo.

“Hawa polisi wajue kitu kimoja, wewe unaweza kuwa OCD leo, mimi leo naweza kuwa Mbunge napiga maneno tu, au mwingine akawa Mbunge, lakini kesho mimi ndiye Rais – ndiye ninateua IGP, ndiye ninayeamua pensheni zenu. Polisi wekeni akiba,” amesema

Zitto amesisitiza kuwa CCM haitadumu madarakani milele, akisema kuwa muda wake umekwisha, na kwamba mfumo wa kidemokrasia unaruhusu mabadiliko ya mamlaka kwa njia ya kura.

Katika kuwatia moyo vijana wa polisi waliopo kazini, Zitto amewataka wasikubali kufuata maagizo ya wakubwa wao yanayokinzana na misingi ya haki, akisema wao ndio viongozi wa usalama wa baadaye.

Post a Comment

Previous Post Next Post