Na Mapuli Kitina Misalaba
Zoezi la uokoaji katika machimbo ya Nyandolwa wilayani
Shinyanga linaendelea, ambapo hadi sasa watu 11 wametolewa kati ya wachimbaji
25 waliofunikwa na mgodi Agosti 11, mwaka huu 2025.
Kati ya waliotolewa,
watatu wameokolewa wakiwa hai na nane wakiwa wamefariki dunia, huku juhudi za
kuwapata wachimbaji wengine 14 zikiendelea kwa kutumia mashine za utambuzi wa
ardhini ili kubaini walipo.
Mnamo Agosti 16, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, aliagiza Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga, Dkt. Kalekwa Kasanga, kuweka ofisi ya muda ya mtendaji
wa kijiji katika eneo la tukio kwa ajili ya kusajili wageni na kuratibu huduma
zinazotolewa na serikali.
Aidha, Agosti 18, 2025
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, alielekeza familia ambazo ndugu zao
bado hawajaokolewa kuteua wawakilishi wachache watakaobaki eneo la tukio ili
kurahisisha utaratibu wa serikali kuwapatia mahitaji muhimu.
Leo Agosti 23, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi,
akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu
Hassan, ametoa maagizo kwa viongozi wa serikali waliopo eneo la ajali kushiriki
kikamilifu kwenye taratibu za mazishi ya waathirika na kuwasilisha rambirambi
za Rais katika familia husika.
GUSA LINK HAPA CHINI👇
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment