" SIMBA SC KUZINDUA JEZI ZAKE MPYA SUPER DOM KISHUA

SIMBA SC KUZINDUA JEZI ZAKE MPYA SUPER DOM KISHUA

 

Klabu ya Simba SC imetangaza kuwa itazindua jezi zake mpya za msimu wa 2025/26 kwa mtindo wa kipekee na tofauti na ilivyozoeleka.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema uzinduzi huo utafanyika tarehe 27 Agosti 2025 saa 1:00 usiku katika ukumbi wa Super Dome, Masaki.

Alisema safari hii Simba imeamua kuandaa tukio la hadhi kubwa kutokana na kuwa na mdhamini mpya wa jezi, kampuni ya JayRutty, kwa kushirikiana na kampuni ya kimataifa ya michezo Diadora.

“Tumeamua kufanya tukio la kipekee lenye mvuto kwa jamii na kibiashara. Uzinduzi huu utawakutanisha wadau wakubwa wa Simba na mashabiki watakaonunua jezi baada ya kuzinduliwa,” alisema Ahmed Ally.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, siku hiyo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali, bendi ya muziki (live band), pamoja na vinywaji na vyakula vya kutosha.

Aidha, mgeni rasmi atakuwa ni mchezaji wa zamani bora barani Afrika, anayetambulika duniani kwa mafanikio makubwa katika soka. Mchezaji huyo ndiye atakayezindua jezi hizo rasmi.

Ahmed Ally aliongeza kuwa yeyote atakayehudhuria tukio hilo atalipa Shilingi 250,000, na baada ya kulipa, mashabiki hao watapewa jezi zote tatu za msimu huu mara moja ndani ya ukumbi.


Post a Comment

Previous Post Next Post