Na Lucas Raphael,TaboraMfuko wa hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma Psssf mkoani imewataka wastaafu Nchini wametakiwa kujisajili kidigitali na PSSSF Kiganjani ili kuepukana na matapeli na mikopo umiza ambapo kupitia mfumo huu mstaafu anaweza kujihudumia kupitia simu yake ya mkononi kwa usalama na UFANISI zaidi.Kauli ilitolewa leo na afisa utekelezaji wa mfuko wa hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma Psssf mkoani Tabora Lusanjo Mwalindu alikuwa akizungumza na waandishi wa wakati wakitoa elimu kwa watumishi wa umma kujisajili kidikital ilikuweza kutumia huduma ya PSSSF mkononi katika badnda la mfuko huo kwenye viwanja vya Nane nane mkoani Tabora.Alisema kwamba ili kuweza kupata huduma kwa haraka na kupunguza muda wa kutembea umbali mrefu kwa wastahafu na watumishi wengine wenye uhitaji wa mfuko huo.Lusanjo aliendelea kueleza kwemba mfumo huo wa PSSSF mkononi ni Rahisi kutumiwa na mtumishi yoyote wa umma pale alipo kwa unarahisisha na kupunguz muda kwa mtumishi husika."Ofisi za mfuko zipo mkoani Tabora na kutoa huduma mbalimbali kwa watumishi wote wa umma waliopo mkoani na wilayani kuwepo kwa mfumo huo kunapunguza muda na Fedha kwa watumishi hao"alisema Lusanjo.Aidha baadhi watumishi wa serikali walifika katika banda la mfuko huo, Emmanuel Madaha alisema kwamba mfuko huo umetibu changamoto kubwa kwa watumishi kwa kuwepo kwa mfumo wa PSSAF mkononi ambayo inapunguza muda na gharama kwa watumishi wa wilayani.Alisema kwamba licha ya kupunguza muda na gharama unachochea maendeleo kwa watumishi hao.Naye mtumishi mwengine anayefanya kazi wakala wa misitu Tanzania (TFS), Thomas Wambura alisema kwamba utaratibu huo n mzuri kwa watumishi wa umma ambao wanaitaji kupata taarifa mbalimbali za mfuko huo .Alisema yeye binafsi aliweza kujaza fumo yake ya kustahafu kwa muda mchache kwa kutuumia Psssf mkononi na kufanikiwa kupata mrejesho mzuri mfumo huo ni bora kuliko ule wa zamani."Wastahafu walionitangulia walikuwa wanatembea na Bahasha kila wakati kwa ajili ya kuweka makaratasi mengi ambayo yanahitajika mara baada ya kustahafu"alisema Wambura tofauti na sasa ambapo karatasi chache zinaitaji tu”alisema WamburaHata hivyo Wambura alitoa wito kwa wastahafu kutumia fedha za mafao watakazolipwa kuzitumia kwa malengo kwani Fadha esa hizo hawaezi kuzipata kwa wingi kiasi hicho na kuwaepuka matapeli wanaotumia ushawishi kuzipata fedha za wastahafu.Mwisho

Post a Comment