" DKT. NCHIMBI KESHO KUWASILI SHINYANGA KWA KAMPENI ZA SIKU MBILI

DKT. NCHIMBI KESHO KUWASILI SHINYANGA KWA KAMPENI ZA SIKU MBILI

Na Mapuli Kitina Misalaba 

Mgombea mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, anatarajiwa kuwasili kesho Jumatano mkoani Shinyanga kwa ajili ya kufanya kampeni za siku mbili mfululizo.

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga, Richard Raphael Masele, amesema maandalizi ya mapokezi na mikutano hiyo yamekamilika na wananchi wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi.

Amesema mara baada ya kuwasili, Dkt. Nchimbi ataanza na mkutano wa kampeni wilayani Kishapu, kisha kuelekea mjini Shinyanga ambapo atahutubia wananchi kuanzia saa sita mchana katika Uwanja wa Jasko, Ngokolo Mitumbani.

Tarehe 4 Septemba 2025, mgombea mwenza huyo ataendelea na ziara yake kwa kufanya mikutano ya hadhara Isaka na Kagongwa kuanzia saa tatu asubuhi, kabla ya kuhitimisha kwa mkutano mkubwa katika eneo la Parking ya Malolo Majengo karibu na Uwanja wa Taifa, Kahama mjini.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post